Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Wednesday, 22 April 2026

NBC NA AZAM TV WAZINDUA “KONA YA NBC”: JUKWAA JIPYA LINALOUNGANISHA SOKA, MAARIFA NA FURSA ZA KIUCHUMI

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Cornel Barnabas (wa pili kulia), Meneja wa Mahusiano ya Umma wa Azam Media, Christina Korosso (katikati), Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya (kushoto), pamoja na Mkuu wa Mikakati wa NBC, Msafiri Shayo (kulia), wakionyesha baadhi ya taarifa muhimu kuhusu kipindi kipya cha uchambuzi wa soka “Kona ya NBC”. Kipindi hicho, kinachoandaliwa na mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC—Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Azam TV, kinalenga kuunganisha burudani, maarifa na fursa za kiuchumi kwa wadau wa soka nchini. Tukio hilo lilifanyika jana jioni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisisitiza kuwa uwekezaji wa benki hiyo kwenye soka unaenda mbali zaidi ya udhamini wa kawaida—unalenga kujenga mfumo endelevu wa kiuchumi unaonufaisha wadau wote wa mchezo huo.

Dar es Salaam, Aprili 21, 2026 — Katika hatua inayodhihirisha mwelekeo mpya wa maendeleo ya soka nchini Tanzania, mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa kushirikiana na Azam TV, wamezindua rasmi kipindi kipya cha uchambuzi wa soka kiitwacho “Kona ya NBC”—jukwaa la kisasa linalolenga kuunganisha burudani, maarifa na fursa za kiuchumi kwa wadau wa mchezo huo.

Uzinduzi huo wa kihistoria ulifanyika jijini Dar es Salaam, ukihusisha wadau mbalimbali wa soka wakiwemo viongozi wa taasisi, wachambuzi wa michezo, wanahabari, pamoja na wachezaji wa zamani na wa sasa. Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Cornel Barnabas, na Meneja wa Mahusiano ya Umma wa Azam Media, Christina Korosso.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Cornel Barnabas aliipongeza NBC kwa mchango wake mkubwa katika mageuzi ya soka la Tanzania, akieleza kuwa uwekezaji huo unaendelea kufungua milango mipya ya fursa kwa vijana na kuimarisha nafasi ya soka katika uchumi wa taifa.

Hafla hiyo ilirushwa mubashara kupitia Azam TV na pia kuoneshwa katika ukumbi wa kisasa wa Century Cinemax, ikionesha namna teknolojia na burudani zinavyoweza kuunganishwa ili kuleta uzoefu mpya kwa mashabiki wa soka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Theobald Sabi alisisitiza kuwa uwekezaji wa NBC kwenye soka unaenda mbali zaidi ya udhamini wa kawaida, akilenga kujenga mfumo endelevu wa kiuchumi.

Kupitia ‘Kona ya NBC’, tunapanua wigo wa thamani katika soka—kuanzia kwa wachezaji, vilabu, vyombo vya habari hadi wafanyabiashara. Huu ni uwekezaji unaolenga ajira, ubunifu na ustawi wa vijana,” alisema.

Aliongeza kuwa tangu mwaka 2023, NBC imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 32.6 katika maendeleo ya soka, ikiwa ni pamoja na udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, ligi daraja la kwanza na ligi za vijana—hatua iliyochochea ushindani na uimara wa kifedha wa vilabu.

Sabi pia alirejea mifano ya kimataifa kama Bundesliga na English Premier League, akibainisha jinsi soka linavyoweza kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi kupitia sekta mbalimbali kama utalii, biashara na ajira.

Kwa upande wake, Christina Korosso alisema ushirikiano huo unalenga kuinua ubora wa maudhui ya michezo nchini na kuongeza ushiriki wa mashabiki.

Kupitia ‘Kona ya NBC’, tunaleta jukwaa linalowaunganisha wadau wa soka—kuanzia uwanjani hadi majumbani. Lengo ni kukuza tasnia ya michezo kwa ujumla,” alieleza.

Naye Cornel Barnabas aliipongeza NBC kwa mchango wake mkubwa katika mageuzi ya soka la Tanzania, akisisitiza kuwa uwekezaji huo unaendelea kufungua fursa kwa vijana na kuimarisha mchango wa soka katika uchumi wa taifa.

Kipindi cha “Kona ya NBC” kitarushwa kupitia Azam Sports HD 1 kila Jumatatu saa 1:00 jioni na kurudiwa Jumanne, kikitarajiwa kuwafikia zaidi ya watazamaji milioni 14 kila wiki.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa NBC, David Raymond, kipindi hicho kitaenda zaidi ya uchambuzi wa mechi kwa kujumuisha simulizi za mafanikio, majadiliano ya fursa za kiuchumi ndani ya michezo, pamoja na kuwapa mashabiki nafasi ya kushiriki.

Kwa mashabiki, “Kona ya NBC” si kipindi cha kawaida bali ni darasa jipya—jukwaa litakalowapa uelewa wa jinsi ya kunufaika na soka nje ya uwanja. Wengi wanaamini kuwa mpango huu utabadilisha mtazamo wa muda mrefu wa kushabikia bila kunufaika kiuchumi, na badala yake kufungua milango ya maarifa, ubunifu na kipato kupitia mchezo huo maarufu.

Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano ya Umma wa Azam Media Christina Korosso alieleza kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuinua ubora wa maudhui ya michezo nchini.





No comments:

Post a Comment