Benki ya NMB imeingia makubaliano ya miaka miwili na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kupitia Benki ya NMB.
Kupitia makubaliano haya:
Kunufaika na mikopo hii, tembelea tawi lolote la NMB lililo karibu nawe.
Kupitia makubaliano haya:
- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 18.5 zitakazokopeshwa kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kupitia Benki ya NMB, kwa masharti nafuu, na kwa riba ndogo ya 7% tu.
- Mikopo hii itakopeshwa kwa wafanya biashara ndogo ndogo waliosajiliwa, na kutambulishwa kwa Benki ya NMB na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
- Kabla ya kuidhinisha mikopo hii, Benki ya NMB itajiridhisha kwa kuwatembelea wafanya biashara hawa katika maeneo yao, ili kuhakikisha mikopo inawafikia walengwa waliokusudiwa.
- Mfanyabiashara atakopeshwa kulingana na mahitaji ya biashara anayoifanya.
- Benki ya NMB kwa kushirikiana na Wizara, itahakikisha wanufaika wanapatiwa elimu ya kifedha, ili kuwajengea nidhamu ya matumizi ya fedha hizi katika kutimiza malengo yaliyokusudiwa na kuweza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Kunufaika na mikopo hii, tembelea tawi lolote la NMB lililo karibu nawe.
No comments:
Post a Comment