Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 31 May 2024

USIKOSE CHAMPIONS LEAGUE FINAL NDANI YA DStv COMPACT


Piga *150*53# kulipia kifurushi cha Compact mapema.

#mfalmewasokanidstv
#sokabiladstvhainogi
#unakosaje

Thursday, 30 May 2024

USIKOSE FAINALI YA UCL DORTMUND vs REAL MADRID NDANI YA DStv COMPACT


SAMSUNG'S CUTTING-EDGE WINDFREE™ AIR CONDITIONERS DELIVER UNMATCHED COMFORT & EFFICIENCY


Nairobi, Kenya: Samsung Electronics has once again raised the bar with its latest range of WindFree™ air conditioners, setting a new standard for innovation and comfort in household climate control.


Over the years, Samsung has earned a reputation for its innovative gadgets and appliances. Its air conditioners are no exception. They blend traditional features with cutting-edge technology like AI and multiple cooling modes, offering various options to suit different needs.


At the heart of these advanced air conditioners is the groundbreaking WindFree™ Cooling Technology. This standout feature promises not just cooling but an unparalleled cooling experience. The Fast-Cooling mode swiftly brings the room to your desired temperature, setting the stage for the transformative WindFree™ Cooling mode.


Here, the air conditioner emits cool air through a remarkable 23,000 micro air holes, creating an atmosphere of 'still air' with minimal movement—just 0.15m/s—eliminating bothersome drafts and ensuring pure comfort. Notably, this mode slashes energy consumption by an impressive 77%, keeping your space and wallet cool.

Eng. Herbert Wamalwa - Heating Ventilation and Air Conditioning Unit Head, Consumer Electronics Division, Samsung Electronics East Africa, said: “The Digital Inverter Boost technology further exemplifies Samsung's commitment to efficiency and sustainability. This technology can achieve up to 73% energy savings by maintaining desired temperatures without constant cycling, a marked improvement over conventional air conditioning systems. Samsung uses neodymium magnets and a twin-tube muffler to enhance performance while reducing noise levels and blending functionality with peace of mind.

Wednesday, 29 May 2024

MKULIMA SINGIDA AIBUKA NA MILIONI 10 ZA NMB PESA WEKA NA USHINDE


Kampeni ya Weka Akiba, Tumia na Ushinde kwa wateja wa akaunti nafuu, rahisi na salama ya NMB Pesa iliyokuwa na zawadi zenye thamani ya Shilingi Milioni 250, imefikia ukomo kwa mkulima na mjasiriamali Emmanuel Amos Kakale wa Mitundu, Singida kuibuka na zawadi kuu ya Shilingi Milioni 10.


NMB Pesa ambayo ni akaunti isiyo na makato ya mwezi inayofunguliwa kwa Shilingi 1,000 tu, ilizinduliwa miezi mitatu iliyopita, ikiambatana na kampeni hii ambayo ilikuwa droo mbalimbali sambamba na matamasha makubwa katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar.


Ukiondoa kitita hicho cha Shilingi Milioni 10 kilichoenda kwa Kakale, droo ya fainali hiyo iliyofanyika Jumatano Mei 29, NMB Tawi la Mbezi Africana, ilishuhudia pia washindi wengine nane wakijinyakulia Shilingi Milioni 3 kila mmoja, huku wengine wakitwaa mashine ya kufulia, TV janja (smart TV) na friji ya milango miwili.


Washindi wengine wa fainali hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kahwili, walijishindia majiko ya gesi, bodaboda tano na pikipiki nane za magurudumu matatu maarufu kama Toyo.

Akizungumza kabda ya droo hiyo, Mkuu wa Mauzo na Mtandao wa Matawi ya NMB, Donatus Richard, alisema Kampeni ya Weka na Ushinde kupitia NMB Pesa ilipata mwitikio mkubwa ilipozinduliwa, hivyo kuifanya benki kutimiza lengo la kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki.

HEINEKEN YAPANUA WIGO ZAIDI, YAZINDUA BIDHAA ZAKE MPYA NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji - Mhe. Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akimpongeza Meneja Mkazi wa Heineken Tanzania - Obabiyi Fagade mara baada ya kutangaza biashara mpya ya kampuni hiyo kufuatia kununua kampuni za Distell Group Holdings Ltd na Namibia Breweries Ltd kwenye hafla iliyofanyika usiku wa jumamosi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Biashara na masoko, wa Heineken Tanzania, Lilian Paschal.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji - Mhe. Prof Kitila Mkumbo (katikati) akizungumza na hadhara wakati wa kutangaza biashara mpya ya kampuni ya Heineken kufuatia kununua kampuni za Distell Group Holdings Ltd na Namibia Breweries Ltd kwenye hafla iliyofanyika usiku wa jumamosi jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Mkazi wa kampuni hiyo - Obabiyi Fagade na Meneja wa Ukuaji na Maendeleo wa kampuni ya Heineken Beverages - Andre Beyers.

Dar es Salaam, Tanzania - Mei 25, 2024; Kampuni inayoongoza duniani ya vinywaji, Heineken® imesherehekea upanuzi wake zaidi wa vinywaji na kutangaza bidhaa mpya ikionyesha orodha za aina mbalimbali za chapa zilizoanzishwa nchini Tanzania katika hafla ya kipekee iliyofanyika jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Mei 25, 2024.

Hii inafuatia kukamilika kwa ununuzi wa kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’).

Waliohudhuria kwenye hafla hiyo ni wageni waalikwa, viongozi wa tasnia na wawakilishi wa vyombo vya habari, pamoja na Mgeni Rasmi, Mhe. Prof. Kitila A.K Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Wageni wengine mashuhuri waliuhudhuria katika kuadhimisha hatua hiyo muhimu kwa Kampuni ya Heineken Beverages Tanzania ilipozindua bidhaa zake za kusisimua katika soko la Tanzania.

Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, alisema: “Kuunganishwa huku kwa biashara yetu hadi kufikia zaidi ya bia ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni yetu nchini Tanzania na ni kielelezo cha imani yetu kama Heineken, katika ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini. Umiliki wa aina mbalimbali za chapa zinazojulikana imetuwezesha kutoa jalada kamili la vinywaji ili kukidhi mahitaji ya watumiaji yanayoendeleza kwa upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia. Pia, inaonyesha ari yetu kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji tukidumisha nyakati za umoja wa kweli. Sasa kuna toleo la kinywaji cha Heineken kwa ajili yako kwa chochote unachohitaji. Uzinduzi huu unaashiria sura ya kuvutia kwetu tunapoendelea kukua na kukidhi soko la Tanzania”.

USIKOSE FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE NDANI YA DStv COMPACT


Piga *150*53# kulipia mapema kifurushi cha Compact ili usipitwe!

#mfalmewasokanidstv
#sokabiladstvhainogi
#unakosaje

NMB BANK INTEGRATED ANNUAL REPORT 2023 IS OUT



NMB Bank Plc has published its Integrated Annual Report for 2023.

The report highlights the Bank’s key strengths, the progress they have made on the execution of their Medium Term Plan, consistent financial and non-financial achievements, and their commitment to touching lives and empowering communities.

The report also provides insight on the progress the Bank has made on scaling up its Sustainability agenda, with focus on financial inclusion, sustainable finance and operations, and climate risk. NMB Bank has provided its commitment to creating positive impact to the communities they serve and the economy at large.

Click here to read the full report: https://bit.ly/4dVm6Om

#NMBCloseToYou

Tuesday, 28 May 2024

FURAHIA UEFA EUROPA CONFERENCE LEAGUE KWA NGUVU YA BUKU 10 TU!


DStv YAJA NA MSEREREKO WA BURUDANI KIDIJITALI

  • Wateja wa DStv sasa kufurahia burudani zote kupitia intanet muda wowote, mahali popote
  • Tamthilia kali, michuano ya ligi za kibabe ulimwenguni, vipindi vya Watoto bila Dishi, Dikoda wala waya
Dar es Salaam Mei 23, 2024: Kampuni inayoongoza nchini kwa huduma za burudani imetambulisha huduma ya kipekee nchini ambayo inaruhusu wateja wa DStv na watanzania kwa ujumla kufurahia burudani kadha wa kadha kupitia intaneti.

Kwa kutumia huduma ya DStv Stream, wateja wa DStv sasa wataweza kufurahia burudani kadha wa kadha kwa urahisi zaidi kupitia intaneti muda wowote mahali popote kupitia vifaa kama simu ya mkononi, laptop au tablet bila ya kumuhitaji kuwa na kisimbuzi wala dishi la DStv.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Masoko MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo alisema, "Siku zote dhamira yetu ni kuwa wabunifu katika kuleta mapinduzi ya masuala ya burudani na teknolojia. Tumekuwa tukitazama kwa makini vikwazo vya mara kwa mara vinavyowazuia wateja wetu wa DStv na watanzania kwa ujumla katika kupata burudani zetu kwa urahisi na uchunguzi huo umepelekea kuja na ufumbuzi wa kibunifu kwa wateja wetu kupitia huduma hii ya DStv Stream”.

DStv Stream ni moja kati ya huduma za kisasa zinazopatikana ndani ya DStv. Huduma hizi ambazo nyingi zinaendana na maisha ya kidijitali zimewezesha DStv kuendelea kuongoza katika gurudumu la utoaji burudani umiliki wa soko la wateja hapa nchini.

Kijiunga na huduma ya DStv Stream mteja atahajitajika kufuata hatua zifuatazo;
  1. Kujisali katika tovuti ya https://dstv.stream/
  2. Pakua application ya DStv Stream katika kifaa chake kisha kuingiza taarifa zake za msingi alizotumia wakati wa usajili kwenye tovuti
  3. Chagua kifurushi ukipendacho
  4. Chagua muda na njia ya kufanya malipo
  5. Furahia huduma yako!
"Tunaahidi kuendelea kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya burudani kidijitali, na siku zote tutaendelea kuwekeza katika teknolojia na hatimaye, kuwafikia watanzania wengi zaidi laikini pia kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi yetu," alieleza Shelukindo.

FURAHIA DStv MSEREREKO BILA DISHI, DIKODA WALA WAYA



Mserereko bila Dishi, Dikoda Wala Waya.

Furahia burudani zote ukiwa na intaneti, muda wowote mahali popote!

#mserereko

FCC & TRADEMARK AFRICA INK £600,000 AGREEMENT TO MODERNISE MARKET REGULATION

Director General of the Fair Competition Commission - Willian Erio (centre) and TradeMark Africa's Tanzania Country Director, Elibariki Shammy (left) sign an agreement to modernise market regulation as well as combat counterfeiting in Tanzania.

Dar es Salaam, Tanzania, 28 May 2024: The Fair Competition Commission (FCC) of Tanzania and TradeMark Africa (TMA) have signed a three-year Partner Support Agreement (PSA) aimed at modernising FCC’s operations and strengthening its ability to regulate competition, consumer protection and combat counterfeit activities effectively. Funded by UK International Development, Ireland, and Norway, the Tzs1.56 billion (£600,000) project is designed to address existing market competition and consumer enforcement challenges in the Tanzanian market, including delays in approving mergers and acquisitions, issues with managing anti-competitive trade practices, and difficulties in enforcing anti-counterfeit measures at borders and ports. This initiative promises to transform the trading landscape in Tanzania, making it more competitive, transparent, and inclusive.


The PSA is expected to deliver significant benefits, such as reduced time and costs associated with trade and investment procedures, a decrease in the prevalence of counterfeit products, and enhanced consumer protection. It marks a critical step towards not only improving FCC’s operational efficiency but also boosting both domestic and foreign investment in Tanzania.


At the signing and launch of the programme, FCC Director General, Mr William Erio, stated, "We welcome this strategic partnership with TradeMark Africa as a significant milestone in our efforts to strengthen regulatory capacity and enforcement. Together, we aim to create a level playing field for businesses, promote market competition, protect consumer interests, and support sustainable economic growth in Tanzania. These goals are in line with sixth phase government priorities of improving business environment."

Friday, 24 May 2024

CRDB BANK FOUNDATION, UNFPA KUSHIRIKIANA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI


Dar es Salaam. Tarehe 23 Mei 2024: Katika kuongeza ujumuishi wa wananchi kiuchumi hasa makundi maalumu, Taasisi ya CRDB Bank Foundation imesaini mkataba wa makubaliano kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kuwawezesha kiuchumi vijana kuanzia miaka 18 hadi 24, waliopo shule na wale ambao wameacha shule kwasababu moja au nyengine.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutia saini mkataba huo wenye thamani ya dola 300,000 za Marekani, sawa na shilingi milioni 800, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa amesema ushirikiano huo unatokana na kufanana kwa malengo na mipango ya pande zote mbili katika kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi.


“Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023, Taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation tumeelekeza nguvu kubwa katika kuanzisha programu za kuwawezesha vijana na wanawake kujumuishwa kwenye mfumo rasmi wa huduma za fedha, kuwapa mafunzo na mitaji wezeshi kupitia Programu yetu ya Imbeju.
Ushirikiano huu na UNFPA unakwenda kuimarisha jitihada hizi na kuwezesha kufikia vijana wengi zaidi,” amesema Tully.

Kama ilivyo kwa CRDB Bank Foundation, UNFPA inatekeleza programu tofauti za kuwainua wananchi kiuchumi, kuwajengea uwezo wa kuzitambua haki zao, kupunguza migogoro ya kifamilia na kijinsia, pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa wanawake, mabinti na vijana azma ikiwa ni kujenga vijana wenye uwezo wa kiuchumi kuzikabili changamoto za kila siku.


Tully amesema ushirikiano huu unawalenga vijana walio masomoni na wale walioshindwa kuendelea na masomo kwasababu mbalimbali, walemavu pamoja na mabinti waliopata ujauzito wakiwa masomoni. Katika utekelezaji wake, amesema wanakusudia kupunguza changamoto za upatikanaji wa ajira, kuwapa elimu ya fedha, kuwapa elimu ya afya ili kupunguza mimba za utotoni, kupunguza ukatili wa kijinsia na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU), katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma.

“Ushirikiano wetu na UNFPA utajikita kwenye maeneo mawili ya msingi. Kwanza ni kutoa elimu na maarifa ya kujitambua kwa vijana walio shule na walioa nje ya shule itakayojumuisha mafunzo juu ya huduma rafiki za afya, unyanyasaji wa kijinsia, na jinsi ya kuepuka na namna ya kuishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Eneo la pili ni kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali kwa vijana na mabinti ili kuwajengea mazingira ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu,” amefafanua Tully.


Kwa upande wake, Mark Bryan Schreiner, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA nchini amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi tofauti inayolenga kuwainua wananchi hasa wa makundi yaliyosahaulika katika jamii ili kuwa na uchumi jumuishi na wanufaika wakubwa wa programu zake ni wanawake, vijana wakiwamo mabinti wenye rika la balehe, na wahamiaji wanaoomba hifadhi kutokana na migogoro ya kisiasa na kijamii inayotokea kwenye mataifa jirani.

DKT NCHEMBA AUSHUKURU UMOJA WA ULAYA KWA KUSAIDIA MAENDELEO YA NCHI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambapo ameushukuru Umoja huo kwa mchango wake katika maendeleo ya nchi kupitia misaada na mikopo yenye masharti nafuu ambapo hadi sasa uwekezaji wa Umoja huo umefikia thamani ya euro bilioni 3 sawa na takriban shilingi trilioni 8 za Tanzania. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Makazi ya Balozi wa Umoja huo, Mhe. Christine Grau, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa mchango wake katika maendeleo ya Tanzania, kupitia misaada na mikopo yenye masharti nafuu ambapo hadi sasa uwekezaji wa Umoja huo umefikia thamani ya euro bilioni 3 sawa na takriban shilingi trilioni 8 za Tanzania.


Dkt. Nchemba (Mb), amesema hayo wakati akiongoza maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya yaliyofanyika katika Makazi ya Balozi wa Umoja huo, Mhe. Christine Grau, Jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa euro bilioni 2.4 sawa na shilingi trilioni 6.4 ni msaada na kiasi kingine cha euro milioni 573 sawa na shilingi trilioni 1.5 ni mkopo wenye masharti nafuu uliotolewa na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (European Investment Bank-EIB) ambazo zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za usafiri, nishati, kilimo, biashara na uwekezaji, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, maji na usafi wa mazingira.


Aidha, Dkt. Nchemba aliishukuru Jumuiya hiyo kwa kutenga kiasi cha euro bilioni 300 kupitia mpango wake wa Global Gateway, kwa ajili ya mikakati ya kukuza uwekezaji ambapo kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 150 zimetengewa nchi za kiafrika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu pamoja na mifumo ya kidigiti.

“Msaada huo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo na utengamano wa nchi zetu, kukuza uchumi, na maendeleo ya wananchi kwa ujumla” alisema Dkt. Nchemba

USIKOSE AL AHLY vs ES TUNIS JUMAMOSI KWA BUKU 10 TU NDANI YA DStv

Pia piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema usipitwe na mechi hii.


#sokabiladstvhalinogi
#mfalmewasokanidstv
#unakosaje

USIKOSE FA CUP FINAL KWA NGUVU YA BUKU 10 TU JUMAMOSI NDANI YA DStv


Pia piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema usipitwe na mechi hii.

#sokabiladstvhalinogi
#mfalmewasokanidstv
#unakosaje

Thursday, 23 May 2024

MKURUGENZI WA PBZ BANK ARAFAT HAJI AKUTANA NA TIMU YA UONGOZI


Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ Bank, Ndg. Arafat Ally Haji, amekutana na kufanya mazungumzo na timu yake ya uongozi wa PBZ Bank ikiwa ni siku yake ya kwanza kuingia ofisini baada uteuzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi. 


Mkurugenzi Arafat alikuwa ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar kabla ya uteuzi huu, ambapo amekuwa akikabidhi majukumu, kabla kuingia rasmi kwenye majukumu mapya kama Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank). 


PBZ Bank ni Miongoni mwa mabenki makubwa Tanzania, ikiwa na Rasilimali za Trilioni 2.05, Amana Trilioni 1.73, na Faida kabla ya kodi ya Bilioni 75.2 kwa mujibu wa hesabu za Mwaka 2023, ikiiweka benki kwenye nafasi ya 7 miongoni mwa Mabenki 44 yaliopo Tanzania.

FURAHIA FA CUP MAN CITY vs MAN UNITED KWA NGUVU YA BUKU 10 TU!!!


VODACOM NA SAMSUNG WAZINDUA 'MILIKI SIMU, LIPA MDOGO MDOGO'

George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania (kushoto) na Edwin Byampanju, Mwakilishi wa Samsung Tanzania wakiwa katika uzinduzi wa mpango ujulikanao kama ‘Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo’ ambao unamwezesha mteja wa Vodacom kulipa kiasi kidogo cha fedha na kumiliki simu janja huku akiendelea kupunguza deni lake kidogo kidogo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, tukio hilo limefanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania mnamo tarehe 21 May 2024 jijini Dar es Salaam.
  • Lengo mojawapo la Vodacom Tanzania PLC ni kuhakikisha tunaipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, na hili litafikiwa kwa kuwaletea Watanzania intaneti yenye kasi na ubora wa hali ya juu, lakini pia hii inatakiwa iende sambamba na vifaa thabiti.
  • Kama mnavyojua sasa hivi Sisi ni Zaidi ya Mtandao, kwa maana kwamba huduma na bidhaa zetu zimevuka Kiwango cha kuwa mtandao tu, tunafanya vitu na kutoa huduma ambazo ni Zaidi ya Mtandao.
  • Katika muendelezo wa kuhakikisha kila mtanzania anamiliki SIMUJANJA na anaingia katika ulimwengu wa kidigitali, leo tunatambulisha kwenu aina nne mpya za simu ambazo mteja wetu wa Vodacom ataweza kupata katika maduka yetu, kupitia mfumo wetu wa mkopo wa simu(Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo).
  • Lakini pia kupitia menu yetu ya *150*00*44# mteja ataweza kuangalia aina ya simu ambayo ataweza kukopa na malipo ya awali atakayotakiwa kulipia ili kuchukua simu kwenye maduka yetu.
Simu ambazo tumeziongeza ni pamoja na Neon Ultra, Samsung A05, A05s na A15. Mteja ataweza kujipatia:
  1. Neon Ultra kwa kianzio cha TZS, 30,000 na kulipia kila siku TZS 1,000 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  2. Samsung A05 kwa kianzio cha TZS, 45,000 na kulipia kila siku TZS 1,400 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  3. Samsung A05s kwa kianzio cha TZS, 55,000 na kulipia kila siku TZS 1,800 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  4. Samsung A15 kwa kianzio cha TZS, 70,000 na kulipia kila siku TZS 2,200 nakufurahia 200MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
Sote tunafahamu kwamba kwa sasa simu Sio anasa, bali ni kitu cha muhimu sana kuwa nacho, mbali na kuitumia kama chombo cha mawasiliano lakini mtu anaweza kuitumia kama kitendea kazi.

Wednesday, 22 May 2024

KAMPUNI YA HEINEKEN YATANGAZA UJIO WA BIDHAA MPYA TANZANIA

Meneja Mkazi wa Heineken Tanzania, Obabiyi Fagade (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu maandalizi uzinduzi wa bidhaa zao mpya kufuatia kununua kampuni ya Distell na Namibia Breweries ambao utatangazwa jumamosi wiki hii. Wengine kulia ni Mkuu wa Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Lilian Paschal na Mkuu wa Mauzo, Amani Kimaro.

Dar es Salaam, Tanzania, Mei 22, 2024 – Kampuni inayoongoza duniani ya kutengeneza vinywaji, Heineken, leo imetangaza rasmi kuzindua rasmi jarida lake jipya la Vinywaji vya Heineken kwa waandishi wa habari nchini Tanzania kufuatia kukamilika kwa hivi karibuni kwa kampuni hiyo kununua Distell Group Holdings Limited ('Distell') na Namibia Breweries Limited ('NBL').

Bidhaa zao mpya za aina nyingi ambazo zinafanya kazi chini ya jina la 'HEINEKEN Beverages,' inaonyesha dhamira ya kampuni ya kuwasilisha vinywaji vya ubora wa juu kwa watumiaji mbalimbali barani kote.

Meneja Mkazi Nchini wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade, alitoa maoni yake akisema: “Ununuzi wa hivi majuzi ambao unaongeza zaidi ya Euro bilioni 1 katika mapato halisi na Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji kwa nyayo zetu za Afrika bila shaka utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Tumepewa nafasi ya kipekee sio tu kufikia hadhira pana zaidi kutokana na upanuzi huo, lakini pia kutengeneza nafasi nyingi za kazi na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi.”

Heineken, sasa inapatikana katika masoko 114 na kuuzwa katika zaidi ya masoko 180 na iko tayari kuwa kiongozi wa soko katika tasnia ya vinywaji nchini Tanzania. Ikiongozwa na maadili yake ya msingi, kampuni imejitolea kuunda nyakati za furaha zaidi kwa wateja wake na watumiaji, kuhamasisha ulimwengu bora kupitia shauku, ubunifu na ufanisi.

Ili kusherehekea hatua hii muhimu, Heineken itazindua jalada lake jipya la bidhaa zilizopanuliwa katika tukio la kipekee baadaye wiki hii.

Mgeni Rasmi wa hafla hiyo anatarajiwa kuwa Mhe. Prof Kitila A.K Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Atajumuika na wageni wengine mashuhuri, viongozi wa tasnia mbalimbali, na wawakilishi wa vyombo vya habari kuadhimisha tukio hili muhimu kwa kinywaji cha Heineken Tanzania.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Lilian Pascal
Heineken- Meneja Masoko wa Biashara
+255 744 149 146
Lilian.Pascal@heineken.com

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA PIKIPIKI 20 ARUSHA KUENDELEZA UTALII


Arusha: Benki ya NMB imekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 65 zitakazosaidia kuimarisha ulinzi mkoani Arusha.


Mchango huo ambao umetolewa kwa Jeshi la Polisi mkoani humo unaendana na mpango mkakati wa benki hiyo wa kuendeleza sekta ya utalii unaolenga kuimarisha mifumo endelevu ya ikolojia ya utalii.


Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda iliyofanyika katika Tawi la NMB Clock Tower jijini Arusha jana, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi alisisitiza dhamira ya benki hiyo kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali kusaidia maendeleo ya sekta ya utalii.


“Kwetu mkoa wa Arusha ni muhimu na ni wakimkakati kwa kuwa ni kitovu cha watalii ndomana leo tupo mahali hapa kukabidhi pikipiki 20 ili kuimarisha usalama. Kama benki, tunaamini kwamba usalama ukiimarishwa, sekta ya utalii itastawi kwa kiwango kikubwa,” alisemaa


Mponzi alionyesha matumaini kuwa juhudi za benki hiyo mkoani Arusha zitakuwa na athari kubwa zaidi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii nchini kote.


"Juhudi zetu zitakuwa chachu ya ukuaji wa sekta ya utalii kwa ujumla. Tunaamini kuwa watalii wakiwa salama hapa Arusha kama kitovu cha utalii, basi watakuwa tayari kwenda kufurahia maeneo utali katika maeneo mengine nchini kama vile Zanzibar,” Mponzi alisisitiza.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Wazawa nchini Samuel Diah wakati wa hafla hiyo aliipongeza Benki ya NMB kwa mchango huo akionyesha imani kuwa kwa kiasi kikubwa utachochea ukuaji wa sekta ya utalii mkoani humo.


“Kwa kweli mchango huu umekuja wakati muafaka kwani kuhakikisha usalama wa watalii wa ndani na nje ni kipaumbele kikuu kwetu kwa sasa. Juhudi za Benki ya NMB zitahakikisha usalama wa mkoa wa Arusha wakati wote na vile utachangia juhudi za Serikali ya awamu ya sita za kukuza sekta ya utalii,” alisema Diah.

ECOBANK LAUNCHES NEW LOAN SERVICE FOR CIVIL SERVANTS


Ecobank Tanzania has officially launched a new loan service specifically for civil servants. This initiative aims to help all civil servants in the country achieve their goals quickly and easily.


Key Highlights:
  • Loans up to TZS 125 million
  • Low interest rate of 12%, with a repayment period of up to 7 years
  • Quick loan processing within 24 hours
  • Free Civil Servant Account with no monthly fees
  • Life Insurance cover for the borrower
  • Option to buy out loans from other financial institutions
Ecobank Tanzania is committed to improving the financial wellbeing of civil servants across various sectors. Visit our branches in Dar es Salaam, Arusha, and Mwanza to take advantage of this service. We look forward to serving you.

For more information:

Phone: 0800110021
Email: ecobanktz@ecobank.com

#EcobankTanzania #CivilServantsLoan #FinancialServices #DarEsSalaam #Arusha #Mwanza

ECOBANK YAZINDUA MIKOPO KWA WATUMISHI WA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya utoaji wa Mikopo kwa Watumishi wa Umma hapa nchini iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Ruth Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kuwahudumia Watumishi wa Umma watakaohitaji mikopo ya Ecobank Tanzania wakati wa hafla iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Ecobank Tanzania imezindua huduma ya utoaji wa Mikopo kwa watumishi wa umma ambayo inawalenga watumishi wote wa umma nchini ili kufikia malengo yao ambayo wamejiwakea na kuyakamilisha kwa uharaka na urahisi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu amesema ni wakati sasa kwa benki hiyo kuwafikia watumishi wa Umma katika sekta mbalimbali nchini na kuwapatia huduma hii muhimu sana ya Mikopo ili kuinua vipato na maisha yao kwa ujumla.

"Si hivyo tu bali kwa watumishi wa umma ambao tayari wana mikopo kupitia taasisi zingine ya fedha, Ecobank itanunua mkopo yao na kuwapa nafasi ya kuongeza zaidi ili kuyafikia malengo yao." Alisema Asiedu.

Naye Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Bi. Ruth Mwaiselage amesema Ecobank Tanzania itatoa mikopo ya hadi millioni 125 kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Serikali kwa riba ndogo kabisa ya asilimia kumina mbili (12% tu) ambapo mtumishi wa umma anaweza kukipa katika kipindi kisichozidi miaka saba. Mikopo hii itatolewa kwa haraka ndani ya masaa 24.

FAINALI ZOTE MUBASHARA DStv KWA NGUVU YA BUKU 10 TU!!!


MWANGA HAKIKA BANK YAZINDUA HUDUMA YA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI

Mkuu wa Idara ya Mikopo - Yonah Mgongolwa (kushoto), Mkuu wa Idara ya Wateja Wadogo na Wakati Benki ya Mwanga Hakika - Mwinyimkuu Ngalima (katikati) na Mkuu wa Idara ya Biashara kwa Wateja Wakubwa - Projest Massawe.
  • Wajasiliamali wadogo na wa kati kupata mkopo wa Fursa wenye gharama nafuu na dhamana rahisi zinazolingana na aina ya biashara zao
  • Huduma hiyo inakuja na akaunti ya malengo ili kuwasaidia kuhifadhi pesa kwa urahisi
Dar es Salaam: Katika azma yake ya kuwezesha biashara nchini, Benki ya Mwanga Hakika imeleta sokoni huduma ya mikopo rahisi kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuwakwamua kiuchumi ijulikanayo kama Fursa Loan.

Huduma hiyo ya kipekee inakuja wakati ambapo watanzania wengi wamekuwa wakihitaji huduma za mikopo yenye riba nafuu na dhamana zinazoendana na aina ya biashara zao.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, leo Jumatano 22 Mei, 2024, Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa Mwanga Hakika Bank, Mwinyimkuu Ngalima alisema benki hiyo imejizatiti katika kuleta huduma zinazokidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya wateja.

“Tunafarijika kuja na huduma hii ya mkopo kwa wajasirimali wadogo na wa kati ambayo ni mikopo yenye gharama nafuu na dhamana zake zinalingana na aina ya biashara zao.

“Tunaamini huduma hii inaenda kuwa msaada mkubwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kama mamalishe, bodaboda, madereva tax na wengineo ambao wamekuwa wakishindwa kupata mikopo kutokana na gharama kubwa na kutokuwa na dhamana,” alisema.

Ili mteja aweze kupata mkopo kwenye benki anahitaji kuwa na dhamana ya mali isiyohamishika kama vile nyumba zenye hati miliki au mashine (kiwanda) jambo ambalo limekuwa likiwakosesha mikopo hasa wafanyabiashara wadogo wasio na dhamana hizo.