Mkurugenzi Arafat alikuwa ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar kabla ya uteuzi huu, ambapo amekuwa akikabidhi majukumu, kabla kuingia rasmi kwenye majukumu mapya kama Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank).
PBZ Bank ni Miongoni mwa mabenki makubwa Tanzania, ikiwa na Rasilimali za Trilioni 2.05, Amana Trilioni 1.73, na Faida kabla ya kodi ya Bilioni 75.2 kwa mujibu wa hesabu za Mwaka 2023, ikiiweka benki kwenye nafasi ya 7 miongoni mwa Mabenki 44 yaliopo Tanzania.
No comments:
Post a Comment