- Wateja wa DStv sasa kufurahia burudani zote kupitia intanet muda wowote, mahali popote
- Tamthilia kali, michuano ya ligi za kibabe ulimwenguni, vipindi vya Watoto bila Dishi, Dikoda wala waya
Kwa kutumia huduma ya DStv Stream, wateja wa DStv sasa wataweza kufurahia burudani kadha wa kadha kwa urahisi zaidi kupitia intaneti muda wowote mahali popote kupitia vifaa kama simu ya mkononi, laptop au tablet bila ya kumuhitaji kuwa na kisimbuzi wala dishi la DStv.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Masoko MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo alisema, "Siku zote dhamira yetu ni kuwa wabunifu katika kuleta mapinduzi ya masuala ya burudani na teknolojia. Tumekuwa tukitazama kwa makini vikwazo vya mara kwa mara vinavyowazuia wateja wetu wa DStv na watanzania kwa ujumla katika kupata burudani zetu kwa urahisi na uchunguzi huo umepelekea kuja na ufumbuzi wa kibunifu kwa wateja wetu kupitia huduma hii ya DStv Stream”.
DStv Stream ni moja kati ya huduma za kisasa zinazopatikana ndani ya DStv. Huduma hizi ambazo nyingi zinaendana na maisha ya kidijitali zimewezesha DStv kuendelea kuongoza katika gurudumu la utoaji burudani umiliki wa soko la wateja hapa nchini.
Kijiunga na huduma ya DStv Stream mteja atahajitajika kufuata hatua zifuatazo;
- Kujisali katika tovuti ya https://dstv.stream/
- Pakua application ya DStv Stream katika kifaa chake kisha kuingiza taarifa zake za msingi alizotumia wakati wa usajili kwenye tovuti
- Chagua kifurushi ukipendacho
- Chagua muda na njia ya kufanya malipo
- Furahia huduma yako!
No comments:
Post a Comment