Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Wednesday, 29 May 2024
HEINEKEN YAPANUA WIGO ZAIDI, YAZINDUA BIDHAA ZAKE MPYA NCHINI
Dar es Salaam, Tanzania - Mei 25, 2024; Kampuni inayoongoza duniani ya vinywaji, Heineken® imesherehekea upanuzi wake zaidi wa vinywaji na kutangaza bidhaa mpya ikionyesha orodha za aina mbalimbali za chapa zilizoanzishwa nchini Tanzania katika hafla ya kipekee iliyofanyika jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Mei 25, 2024.
Hii inafuatia kukamilika kwa ununuzi wa kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’).
Waliohudhuria kwenye hafla hiyo ni wageni waalikwa, viongozi wa tasnia na wawakilishi wa vyombo vya habari, pamoja na Mgeni Rasmi, Mhe. Prof. Kitila A.K Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Wageni wengine mashuhuri waliuhudhuria katika kuadhimisha hatua hiyo muhimu kwa Kampuni ya Heineken Beverages Tanzania ilipozindua bidhaa zake za kusisimua katika soko la Tanzania.
Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabiyi Fagade, alisema: “Kuunganishwa huku kwa biashara yetu hadi kufikia zaidi ya bia ni hatua muhimu katika ukuaji wa kampuni yetu nchini Tanzania na ni kielelezo cha imani yetu kama Heineken, katika ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini. Umiliki wa aina mbalimbali za chapa zinazojulikana imetuwezesha kutoa jalada kamili la vinywaji ili kukidhi mahitaji ya watumiaji yanayoendeleza kwa upanuzi wa kinywaji cha Heineken zaidi ya kinywaji cha bia. Pia, inaonyesha ari yetu kutokana na uzoefu wa kipekee kuhudumia watumiaji wa Kitanzania ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji tukidumisha nyakati za umoja wa kweli. Sasa kuna toleo la kinywaji cha Heineken kwa ajili yako kwa chochote unachohitaji. Uzinduzi huu unaashiria sura ya kuvutia kwetu tunapoendelea kukua na kukidhi soko la Tanzania”.
Akitoa pongezi kwa kinywaji cha Heineken® kwenye uzinduzi wa biashara na huduma yake mpya, mgeni rasmi Mhe. Prof. Kitila A.K Mkumbo, Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji alisema “Nimefurahi kushuhudia uzinduzi wa Ofisi mpya ya Heineken nchini Tanzania. Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji wa Tanzania na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu na kuongeza ajira. Kujikita kwa Heineken kwenye soko letu ni dhahiri, na ninatazamia kuona matokeo chanya ya jalada lao jipya iliyopanuliwa kwa uchumi na watu wetu.”
Uzinduzi wa biashara mpya ya Heineken pamoja na bidhaa mpya zinazopatikana nchini Tanzania ni hatua muhimu kwa Heineken Beverages International ni sehemu ya mipango yake kupanua biashara na uwekezaji wa kimkakati. Heineken inatoa shukrani zake kwa wageni, washirika, na wafuasi wote kwa kujumuika katika sherehe hii, wakitazamia safari ya kusisimua mbeleni.
Kwa Maelezo Zaidi tafadhali wasiliana na:
Lilian Pascal
Heineken- Meneja Masoko wa Biashara
+255 744 149 146
Lilian.Pascal@heineken.com
Kuhusu Heineken:
Heineken ni moja wapo ya kampuni kuu za vinywaji ulimwenguni, iliyojikita kusambaza bidhaa za hali ya juu kwa watumiaji kote ulimwenguni. Kwa uwepo katika masoko 114 pamoja na zaidi ya masoko 180 ya mauzo, Heineken inaendelea kupanua jalada lake ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment