Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akisalimiana na Rais wa Benki ya Dunia, Ajaypal Singh Banga. |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ameshiriki uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika kwa siku tatu Zanzibar.
Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar - Hemed Suleiman Abdalla, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mhe. Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Emmanuel Tutuba na viongozi wengine.
No comments:
Post a Comment