Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 6 November 2023
Y9 MICROFINANCE YAWAZAWADIA WASHINDI WA DROO
Dar es Salaam - Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imekabidhi Bi. Ummy Kuruthumu mkazi wa Zanzibar zawadi yake ya simu janja baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya kampeni ya pakua app ya Y9 Microfinance na kupata huduma ya tatu ambazo ni mkopo wa fedha taslimu.
Ummy alikabidhiwa zawadi hiyo na Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya ambaye pia alieleza kuwa hii ni fursa kubwa sana kwa watanzania kwani Taasisi ya Y9 imekuja kuwa mkombozi kwa watanzania hata wale wenye kipato cha chini.
Mang’enya pia amewapongeza washindi wote kwa kujiunga na huduma zao na kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo simu, pikipiki vilevile ameongeza kwamba kwenye droo ya mwisho ambayo itanyika katikati ya mwezi Disemba kutakuwa na zawadi kubwa zaidi ya gari aina ya Toyota IST.
Alisema kuwa washindi hao wameshinda zawadi hizo baada ya kupakuwa App yetu na kukopa kupitia app na kurejesha mikopo yao ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu zetu.
Alisema kuwa zawadi bado zipo nyingi na kuwaomba Watanzania kuendea kutumia huduma zao. “ Tumekuwa na muendelezo wa kuchezesha droo kila wiki na na kutoa zawadi kila wiki kwa washindi wetu leo pia tumechezesha droo ambapo tumepata washindi wawili kutoka mikoa ya Rukwa, Bwa Boniface Senga ambae amejishindia simu janja na mshindi wapili ni Bwa Iddi Kiluvia kutoka Njombe ambae amejishindia pikipiki.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Salim Mkufi aliwapongeza washindi hao kwa kuiamini Taasisi ya Y9 na kuwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yao.
Mkufi pia ameipongeza Taasisi ya Y9 kwa namna ilivyoweza kuwafikia vijana wengi wa kitanzania na kuwapa mikopo kwa masharti rafiki na kuwataka waendelee kuongeza wigo kutanua huduma zao ila kila mtanzania anufaike na mikopo hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment