Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Wednesday, 25 October 2023
TIGO YAZINDUA 'TIGO PESA RAFIKI'
Dar es Salaam, 24 Oktoba 2023: Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania, Tigo Tanzania, leo imetangaza ubunifu kwa wateja kufanya miamala yao ya Tigo Pesa kupitia jukwaa la WhatsApp liitwalo Tigo Pesa Rafiki. Chaguo hili jipya la miamala kupitia programu inayomilikiwa na Meta, ni la kwanza sokoni na litawawezesha wateja kufanya miamala kadhaa, yote ndani ya ukurasa wa WhatsApp unaofahamika zaidi.
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa,Angelica Pesha, ameelezea shauku yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tigo Pesa Rafiki, Anasema, "Tunafurahia kuwaletea Watanzania Tigo Pesa Rafiki, tukionesha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la kibunifu na rafiki ambayo itaboresha maisha ya kila siku ya wateja wetu. Huduma hii itarahisisha miamala ya kidijitali na kuharakisha ujumuishaji wa kifedha kote Tanzania."
“Kama kampuni ya mawasiliano ya kwanza kutoa huduma hii ya kibunifu, Tigo inathibitisha kujitolea kwake kwa maendeleo ya kidijitali ambayo yanawezesha ukuaji wa kifedha, kurahisisha malipo, na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini. Hatimaye, lengo la Tigo Pesa Rafiki ni kutoa urahisi kwa wateja kulipa bila matatizo. Tigo Pesa imejitolea kuendesha ushirikishwaji wa kifedha na kidijitali huku ikiboresha uzoefu wa mtumiaji kupitia ubunifu endelevu. Kuunganishwa kwa huduma za Tigo Pesa Rafiki na WhatsApp ni uthibitisho tosha wa dhamira hii.” Ameyasema hayo Pesha
“Ili kupata huduma za Tigo Pesa Rafiki kwenye WhatsApp, wateja wanahitaji tu kusajili nambari zao za simu za Tigo Pesa, barua pepe na namba ya siri. Muunganisho huu unaleta kasi ya Tigo Pesa kwa urahisi kwenye WhatsApp, na kufanya miamala kuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali. Zaidi ya hayo, Tigo Pesa WhatsApp itasimamia fedha na miamala ya wateja wetu moja kwa moja kutoka kwenye chati yako ambayo tayari unapenda kutumia hivyo kurahisisha maisha yako” Pesha alieleza
Anachotakiwa kufanya mteja wa Tigo ni kuhifadhi nambari ya Tigo Pesa Rafiki 0675 300 300 kwenye kifaa chake na kuanzisha chati kwenye WhatsApp, ambapo itakuhimiza kusajili nambari yako ya simu ya Tigo Pesa na kufuata utaratibu rahisi kukamilisha muamala wako. Miamala itakayofanywa kupitia Tigo Rafiki ni pamoja na malipo ya serikali, malipo ya Wafanyabiashara (Lipa Kwa Simu) na miamala ya rafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment