Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 3 October 2023

BETPAWA KUWASAIDIA WATANZANIA 20 KUTIMIZA NDOTO ZAO

Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania - Borah Ndanyungu (kulia) akimwonyesha mwandishi wa Mwananchi - Hellen Hartley namna ya kushiriki kutuma wazo la mradi wakati wa uzinduzi wa Programu ya Dream Maker awamu ya pili iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam. Kupitia programu hii, Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BetPawa Tanzania, imezindua awamu ya pili ya programu yake ya kuwasaidia Watanzania wenye mawazo chanya kutimiza ndoto zao inayojulikana kama ‘Dream Maker’.

Kupitia awamu ya pili ya programu hiyo, jumla ya Watanzania 20 wenye mawazo ya miradi yenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na jamii inayowazunguka, watashikwa mkono na BetPawa na hivyo kutimiza ndoto zao.


Afisa Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubashiri Tanzania - Jehud Ngolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya Dream Maker inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania. Kupitia program hiyo ya kurudisha kwa jamii, Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili, meneja masoko wa BetPawa Tanzania, Borah Ndanyungu alisema programu hiyo itahusisha mikoa mitatu ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya Dream Maker inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania. Kupitia program hiyo ambayo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii, Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.

“Watu watakaokutana na basi maalum la Dream Maker watakaribishwa kupanda na kujaza form pamoja na kurekodi video kuhusu ndoto zao. Wengine ambao hawatapata fursa ya kukutana na basi, wanaweza kufanya hivyo popote pale walipo na kutuma kwa njia ya mtandao kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker,” alifafanua.

Wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania wakifurahi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa programu ya Dream Maker awamu ya pili. Kupitia program hiyo ambayo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii, Watanzania 20 wataweza kusaidiwa kutimiza ndoto zao kwa ufadhili wa BetPawa.

Kwa mujibu wa BetPawa Tanzania, msimu wa kwanza wa Dream Maker uliofanyika Septemba 2021, uliwezesha ndoto za Watanzania 13 kutimizwa. Ndoto hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mpya, viwanja vya michezo ufunguzi wa biashara mpya ambazo pia zimetengeneza ajira kwa jamii inayozizunguka. Mwaka huu, jumla ya miradi 20 itapata ufadhili.

Borah alieleza kuwa fursa ipo wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na kuwataka wote wenye mawazo ya miradi kujitokeza na kuyawasilisha kwa BetPawa.

“Tunafanya ubashiri kuwa rafiki zaidi kwa kuwapa watu fursa ya kubashiri kwa dau dogo na kushinda kikubwa kisha kutimiza ndoto zao. Hata hivyo, katika programu hii ya Dream Maker, huhitaji kubashiri kabisa kwa kuwa ni ya kila mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi. Tueleze ndoto yako bila kujali ukubwa wake. na sisi tutakusaidia kuitimiza na kukufanya kuwa mmoja kati ya wanufaika 20 wa msimu wa pili,” alifafanua Borah.

Aliongeza kuwa BetPawa itatembelea mikoa hiyo mitatu na magari ya matangazo yatakuwa yakihamasisha watu kujitokeza na kuelezea ndoto zao. Zoezi hili litafanyika katika mikoa tofauti tofauti kila msimu hadi litakapomaliza nchi nzima.

“Lengo la BetPawa Tanzania ni kutoa fursa kwa kila Mtanzania kutimiza ndoto yake,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment