Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 12 October 2023

BENKI YA DUNIA YAIFAGILIA TANZANIA KUSIMAMIA UCHUMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, walipokutana na kufanya mazungumzo, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ambapo ameimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri na mageuzi makubwa ya kiuchumi ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi ambacho Dunia inahangaika na misukosuko inayotokana na athari za UVIKO 19, mizozo ya vita pamoja na kuyumba kwa soko la fedha za kigeni. Kikao hicho kimefanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), wakiwa katika mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, ambapo Benki hiyo imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri na mageuzi makubwa ya kiuchumi ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi ambacho Dunia inahangaika na misukosuko inayotokana na athari za UVIKO 19, mizozo ya vita pamoja na kuyumba kwa soko la fedha za kigeni. Kikao hicho kimefanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa kikao cha Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), walipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, ambapo alifafanua namna Serikali ilivyojipanga kusimamia mipango yake mbalimbali ya kiuchumi, Kikao hicho kimefanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb) (kushoto) ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika picha na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb) (kulia) ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (katikati) ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Zarau Kibwe (wa kwanza kulia) na kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Venuste Ndikumwenayo.

Na Benny Mwaipaja, Marrakech, Morocco.

Benki ya Dunia imeendelea kuimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri na mageuzi makubwa ya kiuchumi ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi ambacho Dunia inahangaika na misukosuko inayotokana na athari za UVIKO 19, mizozo ya vita pamoja na kuyumba kwa soko la fedha za kigeni.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, walipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco.

Walisema kuwa mageuzi makubwa ya kiuchumi, kisera na kisheria yanayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yameifanya nchi kuwa na utulivu wa kiuchumi huku wakitarajia uchumi utaendelea kuimarika zaidi baada ya Serikali kufanya maboresho makubwa ya sera mbalimbali ikiwemo ya kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kupitia sekta binafsi.

Pongezi hizo zinakuja siku moja baada ya Ripoti ya Mapitio ya Uchumi iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kubashiri kuwa kutokana na vigezo vyote vilivyotumika kupima mwenendo wa ukuaji wa uchumi katika Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, uchumi wa Tanzania utakua kutoka asilimia 4.7 iliyorekodiwa mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 6.1 mwaka 2024 na kuwa nchi ya pili kwa ukuaji wa uchumi katika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Viongozi hao waandamizi wa Benki ya Dunia, walipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi.

Akizungumza katika Mikutano hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, anayeongoza ujumbe wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania. Alifafanua pia kuwa uchumi wa Tanzania unatarajia kukua kwa wastani wa zaidi ya asilimia 6.0 katika kipindi cha muda wa kati (2024 – 2026).

Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia sera za kiuchumi na kifedha, ikiwemo kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara pamoja na kuishirikisha kikamilifu sekta binafsi katika kuendesha uchumi wa nchi.n

Katika kipindi cha miaka sita kuanzia mwaka 2018 hadi kufikia mwezi Septemba 2023, Benki ya Dunia imeipatia Serikali mikopo nafuu yenye thamani ya jumla ya dola za Marekani bilioni 8.304 sawa Shilingi trilioni 20.358 ili kusaidia utekelezji wa miradi mikubwa ya maendeleo zaidi ya 28 ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi na kukabiliana na hali ya umasikini katika jamii.

No comments:

Post a Comment