Dar es Salaam: Benki ya Letshego Faidika imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la KOPA TUKUBUSTI yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bank, Baraka Munisi alisema kuwa “lengo kubwa ya kampeni hiyo ni kuwafaidisha wateja wao. Alisema kuwa ubunifu walioufanya utawawezesha kuinua vipato vya wateja na kumudu gharama mbalimbali za maisha.”
Baraka Munisi alisema kuwa “benki yao inawajali wateja wao na kuamua kuanzisha kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu (siku 90).”
Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika, Asupya Nalingigwa alifafanua kuwa watakuwa wanafanya droo ya kutafuta washindi kila baada ya wiki mbili ambapo jumla ya washindi 30 watazawadiwa zawadi mbalimbali.
“Kampeni hii ina lengo la kuwawezesha au kuwafaidisha wateja wetu, ambapo zawadi ya kwanza ni kiwango cha fedha cha asilimia 50 ya fedha ya mkopo ambapo mteja wetu alikopa. Pia tutakuwa na zawadi nyingie za fedha taslimu, pikipiki, fulana na shajara (Diary),” alisema Asupya Nalingigwa.
Kwa mujibu wa Bw. Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.
“Pia mteja ambaye ataingia kwenye kampeni hii lazima ajaze fomu maalum ya kukubali vigezo na masharti yaliyowekwa. Tunawaomba wateja wetu kushiriki kwa wingi katika kampeni hii yenye lengo la kuwafaidisha. Benki yetu inawajali wateja wake na kuanzisha kampeni hii kwa ajili yao,” alisisitiza Asupya Nalingigwa.
Benki ya Letshego Faidika ni muunganiko wa taasisi mbili za kifedha za Letshego Tanzania na Faidika na ilianza rasmi shughuli za kibenki mwezi Julai mwaka huu (2023).
No comments:
Post a Comment