Mazungumzo hayo yaliyofanyika Septemba 14, 2023 wizarani - Dodoma yalilenga kuangalia maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili ili kufanikisha mradi huo. Mafunzo hayo yanadhaminiwa na Benki ya KCB Tanzania kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi ikiwamo VETA, SIDO na Vyuo vya Maendeleo (FDC).
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Technologia, Prof. Carolyne Nombo aliipongeza Benki ya KCB kwa jitihada inazofanya katika kuwainua vijana hususani katika kuongeza ujuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank, Christina Manyenye alisema mradi huo unatarajia kuanza mwezi Septemba na utafanyika katika Mikoa sita (6) ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Shinyanga, Arusha na Kilimanjaro. Pia, mradi huu utafanyika visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba).
“Tunapenda kuishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinoogia kwa kulipokea vizuri jambo hili ambalo lina manufaa kwa maendeleo ya vijana hapa nchini. KCB Bank tunaamini kwamba tukiwapa mafunzo vijana wanaweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kupitia kujiajiri,” alisema Manyenye na kusisitiza kwamba program hii ni endeleve.
Benki ya KCB Tanzania ni mdau wa maendeleo na imekuwa ikitekeleza mradi wa 2jiajiri toka mwaka 2016 na hadi sasa mradi huo umewanufaisha watanzania zaidi ya 1,500 kwa kuwapa mafunzo ya ufundi stadi na kuwawezesha kuanzisha biashara mbalimbali.
No comments:
Post a Comment