“Lengo la Android daima limekuwa kuwawezesha watu kupitia huduma za kikompyuta. Ufikiaji wa fursa zilizo kwenye intaneti ni muhimu sana kwa ukuaji wa kiuchumi na ujumuishaji wa kijamii katika nchi yoyote ile. Tunaamini kwamba ushirikiano huu utawaleta Watanzania wengi mtandaoni na kuwasaidia kutumia fursa zinazopatikana mtandaoni,” amesema Martin Njoroge, Mkuu wa Android wa Ushirikiano wa Kimajukwaa, Afrika Mashariki.
Kwa upande wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo alisema “Ubia huu wenye tija ni sahihi kabisa kwani Vodacom itawapatia wateja wake mpango wa kulipia simu janja hivyo kuwezesha kupanda daraja na kumiliki simu janja kupitia malipo ya awamu hivyo kufungua uchumi wa kidijitali na kutengeneza fursa za ziada kwa Watanzania. Vile vile, ubia huu unaenda sambamba na ajenda yetu ya ujumuishwaji wa kidijitali al maarufu Teleza Kidijitali”
Kufurahia huduma hii, wateja wa Vodacom watatakiwa kupiga *150*00# > 5 > 5 > 1 # ili kuona kama wanakidhi vigezo na hivyo kujiunga kwenye huduma, baada ya hapo watapokea SMS iliyo na namba ya kumbukumbu. Wateja watachukua simu zao katika maduka ya Vodacom baada ya kulipa kianzio cha hadi Shilingi 20,000. Vodacom itawazawadia wateja wake MB 100, dakika 10 za kupiga mitandao yote na SMS 10 zitakazotumika ndani ya masaa 24 pindi watakapokamilisha marejesho kwa wakati. Iwapo mteja hatafanya marejesho kwa wakati, Vodacom itafunga kifaa hicho. Hali kadhalika, hata wakati simu imefungwa mteja bado ataweza kuwasiliana na huduma kwa wateja, kutumia M-PESA pamoja na aplikesheni ya Kiosk.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo, wateja wa Vodacom wanahimizwa kubonyeza *150*00# > 5 > 5 > 6 au kupiga namba ya huduma kwa wateja kupitia nambari 100 ili kupata maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment