Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 4 August 2023

NMB YATENGA BIL. 20 BBT, YAMWAGA MIKOPO KWA WAKULIMA


Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuwainua vijana na wanawake kupitia mradi wa kuwawezesha kulima, kuvua na kufuga kibiashara (BBT), Benki ya NMB imetenga jumla ya Shilingi bilioni 20 pamoja na kuwaelimisha vijana na wanawake hao namna ya kupata mikopo hiyo.


Pia NMB imetenga Shilingi bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mazao ya wakulima nchi nzima, ambapo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita jumla ya Shilingi bilioni saba tayari zimeishatolewa.


Hayo yameelezwa na Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Bw. Straton Chilongola alipokuwa akimweleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim, alipotembelea banda la benki hiyo katika viwanja vya John Mwakalange jijini Mbeya, yanapofanyika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane.

Chilongola amesema, pamoja na mambo mengine pia benki hiyo inatoa huduma ya mikopo 'NMB Mshiko Fasta' ambapo wakulima wanaweza kukopa kupitia simu za kiganjani hadi Shilingi 500,000 kupitia simu za kiganja bila dhamana wala kufika kwenye matawi ya benki hiyo.

Alieleza kuwa, benki hiyo pia ni ya kwanza nchini kuwawezesha wakulima kupata mikopo kwa riba nafuu ya 9% kwa mwaka na malipo ni kulingana na muda wa mazao.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa ameongozana na Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega aliipongeza NMB kwa masuluhisho mbalimbali waliyonayo kwa wakulima,
na namna benki hiyo inatoa kipaumbele kwenye sekta ya kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa Taifa, na kuzidi kuinua pato la Mtanzania.

No comments:

Post a Comment