| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia ‘PSSSF Pamoja’ ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Wengine kutoka kulia ni, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe. |
No comments:
Post a Comment