#SokaPromax
#Unakosaje
Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Wednesday, 30 August 2023
Tuesday, 29 August 2023
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI SKULI YA MIL. 600 INAYOJENGWA NA NMB
Mradi huo umezinduliwa ikiwa sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), linaloendelea Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, visiwani Zanzibar.
Tamasha hilo lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Agosti 26 mwaka huu, linafanyika chini ya kauli mbiu 'Tuwalinde Kimaadili Watoto Wetu kwa Maslahi ya Taifa,' na linatumika kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akitoa maelezo ya awali ya mradi huo wa Tasani kwa Rais Samia, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, amesema ujenzi huo ambao ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI), ni kati ya jitihada za wazi za benki yake katika kumuunga mkono kufanikisha maendeleo ya elimu nchini.
Bi. Zaipuna alimueleza Dkt. Samia kwamba ujenzi huo utakaojumuisha madarasa matano yatakayochukua wanafunzi 200 kwa mkupuo mmoja, utakamilika Disemba mwaka huu, tayari kabisa kwa Mwaka wa Masomo wa 2024, ambao utaanza Januari mwakani, na kwamba Skuli ya Maandalizi Tasani itakuwa ni shule ya kwanza katika eneo hilo, ikiwa ni ya tatu kwa Makunduchi.
"Ujenzi wa majengo na samani za ndani kama vile viti, meza na madawati, utaigharimu Benki ya NMB Shilingi Milioni 600, ambazo ni sehemu ya faida yetu tunayoitoa kila mwaka kurejesha kwa jamii.
"Mradi huu ulio kwenye eneo la mita za mraba 467, utajumuisha madarasa matano yatakayobeba wanafunzi 40 kila moja, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya Walimu, jiko, vyoo vya walimu, wafanyakazi na wanafunzi, stoo, Mifumo ya Kisasa ya Maji Safi na Majitaka, pamoja na sehemu ya michezo.
"Mheshimiwa Rais, mradi wa Skuli hii ni uthibitisho wa utayari wa NMB kusapoti Serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kuboresha Elimu nchini.
PRESIDENT MWINYI COMMENDS ABSA FOR MEDICAL SUPPLIES
Speaking after the event named 'Wogging Marathon 2023', organized by Amref in collaboration with the Government of Zanzibar under the sponsorship of Absa, President Dr. Mwinyi expressed his recognition and appreciation for the significant support provided by Absa Bank and the organizers of the marathon.
"On behalf of the government, I extend gratitude to Absa Bank Tanzania and urge them to continue collaborating with us to ensure the success of our goals in reducing maternal and child deaths related to childbirth," said President Dr. Mwinyi.
"I am pleased to hear that this campaign spans three years and started last year, with the aim of raising one billion Tanzanian Shillings. The information I have indicates that total commitments of 792 million Shillings have been made so far, with 557 million Shillings already collected," the President added.
EXIM BANK LAUNCHES WOMEN'S EMPOWERMENT PROGRAM
During the launch, the first cohort of 20 aspiring women entrepreneurs graduated and received certificates and cash prizes for the top performers.
The bank’s program takes the shape of an ‘accelerator or incubator’ in which selected women-based startup companies and/or individual entrepreneurs will be helped to develop their businesses through a range of services including training, startup capital and financial facilities to kick start or scale up their businesses.
For Tanzania, the bank’s program aligns with the Tanzania Development Vision 2025 and the Zanzibar Development Vision 2050 and will be a catalyst in enhancing women’s socio-economic welfare.
Speaking during the launch of the WEP program in Dar es Salaam yesterday, the Exim Bank Chief Executive Officer Jaffari Matundu said his bank is committed to increase the integration of sustainability into its business models and approaches to deliver economic, social, and environmental benefits for all its stakeholders.
Monday, 28 August 2023
BENKI YA NBC YASHIRIKI WOGGING YA AMREF ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa tayari kuongoza washiriki wa mbio fupi zilizo ambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar. Pamoja nae pia wapo Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto kwa Rais Mwinyi), Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais Mwinyi) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (kushoto kwa Naibu Hafidh).
Matembezi hayo yalianzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar. |
Zanzibar; Agosti 28, 2023 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wadau wengine kushiriki kwenye mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar.
Kupitia tukio hilo ambalo ni sehemu ya kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 vitakavyotumika kwenye hospitali mbalimbali za Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya visiwani humo.
Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi hayo yaliyoanzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar mwishoni mwa wiki, Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya alisema mbali na mazoezi ya viungo, ushiriki wa benki hiyo ulilenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza na kuepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ambapo bado kiwango cha changamoto hiyo kipo juu.
"Kama ambavyo amebainisha Rais Dk. Mwinyi kwamba takwimu zinaonesha kuna vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017. Hali hiyo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu na tatizo la kukosekana kwa dawa.’’
RAIS MWINYI AZINDUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). |
Sehemu ya wakazi wa Kizimkazi wakifuatilia uzinduzi huo. |
Karibu tukuhudumie. |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa tamasha la Kizimkazi 2023 ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara NBC wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kizimkazi 2023 uliofanyika mwishoni mwa wiki Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.
Zanzibar, 28 Agosti 2023 - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezindua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni jitihada za wadau hao wawili katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.
Hafla ya uzinduzi huo imefanyika mwishoni mwa wiki ikihusisha uwekaji wa jiwe la msingi eneo unapotekelezwa mradi huo ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2023 hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka serikalini akiwemo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Hafidh, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi, viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi pamoja na wakazi wa eneo hilo.
Akizungumzia mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 4.4 ambapo benki ya NBC imechangia kiasi cha Sh milioni 400, Rais Mwinyi pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo muhimu, alisema huo ni adhma ya serikali hiyo kuboresha huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya vyenye hadhi ya kipekee katika baadhi ya maeneo kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika maeneo hayo huku akiyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na eneo la Tumbatu, Fuoni na Kizimkazi.
STANBIC YAHITIMISHA PROGRAM MAENDELEO YA WASAMBAZAJI
Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara, Benki ya Stanbic - Fred Max. |
- Wahitimu 100 WA program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development program' waaswa kutumia Mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao
Wahitimu 100 wa program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' iliyotolewa na Benki ya Stanbic kwa Kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), (Biashara Incubation), wamehitimu program hiyo Agosti 26, 2023, Katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam.
TADB, SELF MF KUTOA BIL. 6 KWA WAKULIMA WADOGO
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wake wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) imeingia mkataba wa Tshs. Bilioni 6 na SELF Microfinance Fund (SELF MF) kwaajili ya kutoa dhamana ya mikopo ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Mkataba ulioingiwa kati ya pande hizi mbili ni utawezesha TADB kuchagiza upatikanaji wa mitaji kwa wakulima kupitia SELF MF. SELF MF watatoa mikopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi na TADB itatoa dhamana ya hadi asilimia 50 kwa mikopo yote. Wachakataji wa mazao wadogo na wakati (SMEs), wakulima wadogo wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi watanufaika kupitia ushirikiano huu kupitia ofisi zote za SELF MF kote nchini.
Akiongea katika hafla fupi ya kutia sahihi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB David Nghambi alisema kupitia mkataba huu, utaiwezesha SELF MF kuongeza wigo wa utoaji mikopo katika sekta ya kilimo hasa wanawake na vijana.
“Mfuko wa SCGS unaosimamiwa na TADB, unasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo. Kupitia ushirikiano wa TADB na taasisi nyingine za kifedha kama SELF MF. Dhamana tunayoitoa inasaidia taasisi hizi za kifedha kuvutiwa na utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. Pia kupitia mitandao ya taasisi hizi za kifedha wakulima wengi hasa walioko vijijini wanafikiwa.
VODACOM FOUNDATION YADHAMINI MBIO ZA MBUZI
Saturday, 26 August 2023
CMSA YAIDHINISHA CRDB KUTOA HATIFUNGANI YA KIJANI
Akizungumza wakati wa kupokea idhini ya kuuzwa kwa hatifungani hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ni furaha kubwa kupata idhini kutoka CMSA kuiuza hatifungani hiyo ambayo lengo lake si tu kupata rasilimali fedha bali kufanikisha utekelezaji wa miradi yenye mrengo wa kuhifadhi mazingira hivyo kushiriki ipasavyo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Kuhusu uwezeshaji wa miradi ya mazingira, Nsekela amesema kwa mwaka jana pekee, Benki ya CRDB ilikopesha jumla ya shilingi trilioni 6.978 ambazo ni sawa na asilimia 26 ya mikopo yote iliyotolewa na taasisi za fedha nchini. Katika fedha hizo, amesema shilingi bilioni 1.44 zilikopeshwa katika sekta ya misitu, kiasi hicho ni sawa na asilimia 55 ya mikopo yote iliyotolewa kwenye sekta ya misitu.
Licha ya jitihada hizo, mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya fedha kuliko uwezo walionao hivyo kutafuta namna rafiki ya kufanikisha suala hilo.
“Kwa kutambua mahitaji yaliyopo, Benki ya CRDB imeona ni muhimu kutafuta vyanzo vipya vya fedha kuwezesha miradi hii. Leo nina furaha kuona jitihada zetu zimezaa matunda kwa CMSA kutupa idhini ya kuuza hatifungani yetu ya kijani (green bond) ambayo itauzwa kwa awamu tano ambapo katika awamu hii ya kwanza tunatarajia kupata shilingi bilioni 55,” amesema Nsekela.
Friday, 25 August 2023
VITA YA MASHEKHE NA WAMAREKANI NDANI YA DStv
Kivumbi cha EPL wikiendi hii ni Liverpool wanaovaana na Newcastle, je ni timu ipi kuchukua point 3?
@dstvtanzania wanakusogezea mtananage huu Live Sebuleni kwako. Hakikisha unalipia mapema kifurushi chako kwa kupiga *150*53# ili usikose burudani hii.
Na Kama hujajiunga na DStv, Piga Sasa 0659 07 07 07 kujiunga Sasa na ofa ya TShs. 59,000/= tu.
@dstvtanzania wanakusogezea mtananage huu Live Sebuleni kwako. Hakikisha unalipia mapema kifurushi chako kwa kupiga *150*53# ili usikose burudani hii.
Na Kama hujajiunga na DStv, Piga Sasa 0659 07 07 07 kujiunga Sasa na ofa ya TShs. 59,000/= tu.
#SokaPromax
#Unakosaje
#Unakosaje
MASTERCARD AND ZANZIBAR e-GOVERNMENT AGENCY COLLABORATE
- The collaboration is the first MoU with eGAZ to support the implementation of their Digital Government Strategy 2023-2027
- MoU to further support the government’s efforts in bringing more people into Zanzibar’s digital economy
The signing of the Memorandum of Understanding (MoU) took place at the launch of the Zanzibar Digital Government Strategy for 2023-2027, led by H.E Hussein Ali Mwinyi, President of the Revolutionary Government of Zanzibar.
The agreement is the first MoU signing by Mastercard aligned with Zanzibar’s digital transformation goals laid out in their Digital Economy Blueprint and Roadmap. The strategy's main objective is Zanzibar’s transformation into a strong digital economy which will secure digital systems, drive innovative information, communication and technology solutions and develop training for digital governance, ultimately reshaping public services.
Under the three-year collaboration, Mastercard will provide technical assistance and expertise to support the Zanzibar government's efforts. This includes setting up a digital transformation team, collaborating with the government's payment portal ZanMalipo to enable digital payments, and launch two million government cards for better access to services and tourism.
"The like-minded collaboration between Mastercard and the Zanzibar e-Government Agency will help power an inclusive, digital economy that benefits everyone, everywhere in Zanzibar. It is a testament to the profound impact of digitization and builds on Mastercard's global experience in enabling digital transformation and demonstrating the value of fostering cross-sector collaboration, fuelling economic growth and facilitating financial and digital inclusion,” said Shehryar Ali, Country Manager, East Africa, Mastercard.
Thursday, 24 August 2023
NBC, TAIFA GAS KUTOA MIKOPO MFUMO WA GESI KWA TAASISI
Dar es Salaam; Agosti 24, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas wameingia makubaliano ya kiutendaji yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula.
Pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia miongoni mwa watanzania, hatua hiyo pia inatajwa kuwa itasaidia kupunguza gharama kubwa zinaelekezwa kwenye matumizi ya nishati miongoni mwa taasisi hizo.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo Elibariki Masuke huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo Devis Deogratius.
Kwa mujibu wa Bw. Masuke hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu zinazolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kuanza na taasisi zinazohudumia watu wengi.
Pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia miongoni mwa watanzania, hatua hiyo pia inatajwa kuwa itasaidia kupunguza gharama kubwa zinaelekezwa kwenye matumizi ya nishati miongoni mwa taasisi hizo.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo Elibariki Masuke huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo Devis Deogratius.
Kwa mujibu wa Bw. Masuke hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu zinazolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kuanza na taasisi zinazohudumia watu wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)