Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara, Benki ya Stanbic - Fred Max. |
- Wahitimu 100 WA program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development program' waaswa kutumia Mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao
Wahitimu 100 wa program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' iliyotolewa na Benki ya Stanbic kwa Kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), (Biashara Incubation), wamehitimu program hiyo Agosti 26, 2023, Katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam.
na baraza la NEEC kwa kutoa mafunzo kwa wahitimu hao kwani changamoto kubwa iliyopo ni jamii kukosa taarifa sahihi za uwekezaji.
Pia Naibu Spika amewaasa wahitimu kutumia elimu waliyoipata kupitia program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' iliyofanikishwa na benki ya Stanbic kwani biashara sio Mtaji ni taaluma kwa sababu biashara nyingi zimekufa sio kwa kukosa mtaji ni kwa kukosa taaluma ya biashara.
Amesema ili kufanikisha program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' waliyoyapata ni lazima kuomba fursa zilizopo katika miradi ya kimkakati ya serikali ikiwa pamoja na kukamata tenda zinazotolewa katika miradi hiyo kwa manufaa ya taifa na biashara zao na kuajiri watanzania.
Akitoa maagizo kwa viongozi mbalimbali wa serikali amesema kuwa wasimamie maslahi ya wajasiriamali wadogo wadogo pale wanapopata tenda kupata malipo yanayostahili na sio kumnyonya mfanyabiashara wa hapa nchini na kumwezesha mwekezaji zaidi au kampuni ya kigeni.
"Maslahi ya watanzania yawe sawa na maslahi ya mtu asiyemtanzania." Ameeleza
Kwaupande wa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa akizungumza katika mahafali hayo, amesema kuwa watanzania na Makampuni yamekuwa yakiongezeka kila mwaka kushiriki katika miradi ya kimkakati nchini.
Akitaja miradi hiyo ni Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere, Mradi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, ujenzi wa barabara na ujenzi wa madaraja.
Amesema kuwa Changamoto kubwa inayowakabili watanzania ni kukosa taarifa sahihi za uwekezaji, namna ya kurasimisha kampuni, kuandaa vitabu vya mahesabu na namna namna ya kuomba tenda na kuweka viambatanisho vinavyotakiwa.
Amesema benki ya stanbic wamewawezesha watanzania hao 100 kwaajili ya kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya kimkakati ya serikali pale inapojitokeza.
Pia amewashukuru benki hiyo kwa kushirikiana na Baraza la NEEC kwa kufanikisha kutoa mafunzo kwa wahitimu. Pia amewapongeza wa hitimu kwa kuhitimisha program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' ya miezi tisa.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya Stanbic, Fred Max amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili wahitimu ni namna ya kuomba tenda mbalimbali zinazotangazwa pia kukosa taarifa sahihi za namna ya kuchangamkia fursa kwenye miradi ya kimkakati ya serikali.
Amesema kuwa wameona tenda nyingi zimekuwa zikichukuliwa na kampuni zinazojirudi au kampuni za kigeni hivyo kwa sasa kampuni mpya zitaanza kuonekana kutokana na watanzania wengi wataanza kuchangamkia fursa hizo.
Kwa Upande wa Wahitimu wa mafunzo hayo wamewashukuru benki ya Stanbic na baraza la NEEC kwa kutenge muda, rasilimali watu, rasilimali fedha na muda wao kutoa mafunzo ili tuu wanufaike wao.
"Tunawashukuru sana sana kwani mimi nilikuwa naomba tenda zaidi ya mara saba kwa mwaka lakini nilikuwa sipata kumbe kunavitu nilikuwa sijui kama ni mhimu wakati wa kuomba tenda...." Amesema Mnufaika Zakia Mohamed
Katika hafla hiyo ya wahitimu 100 kulitanguliwa na mdahalo uliokuwa na wazungumzaji wanne ambao ni John Ulanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kutoka taasisi ya Sekta binafsi (TPSF), Mwenyekiti wa Bodi ya TWCC, Mercy Silla kutoka TWCC, Brendan Maro kutoka Kituo cha Uwekezaji (TIC), Humphrey Simba ambaye ni Mkurugenzi wa Chemba ya Migodi Tanzania (ASNL) na Mwongozaji mjadala kutoka kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment