Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 24 August 2023

NBC, TAIFA GAS KUTOA MIKOPO MFUMO WA GESI KWA TAASISI

Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (kushoto) na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (kulia) wakijipongeza huku wakionesha hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (wa pili kushoto) na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (wa pili kulia) wakisaini hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mahusiano ya kiutendaji kati ya benki hiyo Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (kulia) na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto).
Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mahusiano ya kiutendaji kati ya kampuni hiyo benki na benki ya NBC yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (wa pili kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto).
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo, Elibariki Masuke (wa nne kushoto) huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Devis Deogratius (wa tatu kulia).
Dar es Salaam; Agosti 24, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas wameingia makubaliano ya kiutendaji yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula.

Pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia miongoni mwa watanzania, hatua hiyo pia inatajwa kuwa itasaidia kupunguza gharama kubwa zinaelekezwa kwenye matumizi ya nishati miongoni mwa taasisi hizo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo Elibariki Masuke huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo Devis Deogratius.

Kwa mujibu wa Bw. Masuke hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu zinazolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kuanza na taasisi zinazohudumia watu wengi.

"Kupitia mpango huu ni wazi kwamba sasa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali , magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula wataweza kupata mikopo kutoka NBC ambayo itawawezesha kupata mfumo mzima wa huduma ya Gas kutoka Taifa Gas na kisha kulipa kidogo kidogo kupitia NBC bila kuaathiri muzunguko wa Biashara zao. Wanachotakiwa kufanya ni kufungua akaunti zetu za ‘kua Nasi’ na kisha waweze kupata huduma hii" alibainisha Masuke.

Akifafanua kuhusu akaunti ya Kua Nasi, Bw. Masuke alisema ni akaunti ambayo haina gharama za uendeshaji za kila mwezi, ikiwa na gharama nafuu za ufanyaji wa mihamala huku ikitoa faida hadi asilimia 2 kwa wenye salio zaidi ya Tshs 100,000.

Kwa upande wake Bw. Deogratius alisema kupitia makubaliano hayo, Kampuni ya Taifa Gas imejipanga kuhakikisha inawatengezea mfumo bora wa gas watumiaji nishati hiyo kwenye taasisi mbalimbali sambamba na kutoa elimu ya kina kuhusu gharama na usimamizi bora ili kuwasaidia walengwa waweze kunufaika na huduma bora, kwa ufanisi na usalama huku pia wakipunguza gharama za matumizi ya nishati kwenye taasisi zao.

"Pamoja na kufanya biashara siku zote Taifa Gas msisitizo wetu umebaki kwenye kuunga mkono sera ya mazingira kupitia matumizi ya nishati safi. Hiyo ndio sababu kubwa tunapotekeleza mipango kama hii tunaweka nguvu zaidi katika utoaji wa elimu ili wateja wetu na jamii kwa ujumla waelewe umuhimu wa nishati safi kwa kimazingira, kiuchumi na matumizi sahihi kwa usalama wao,’’ alibainisha.

Hatua hiyo ya NBC na Taifa Gas inakuja ikiwa ni siku chache tu tangu serikali kupitia Waziri wa nishati Bw. January Makamba itoe wito kwa taasisi za fedha nchini kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuangalia namna zinavyoweza kubuni huduma mahususi za kibenki zinazolenga kurahisisha ununuzi na upatikanaji wa vifaa vya nishati safi ya kupikia.

No comments:

Post a Comment