Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi, Anitha Rwehumbiza akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari. |
Viongozi wa SBL wakitoa ishara ya kutangaza rasmi kurejea kileleni kwa bia ya KIBO GOLD. |
Wafanyabiashara mbalimbali wakiburudika na bia hio katika hafla hio iliyofanyika mjini Moshi. |
Kurudi tena kwa bia hii inalenga kudumisha historia ya kipekee kwa Serengeti Breweries (SBL) kutengeneza bia yenye kilele cha ladha ileile bora na adimu ambapo pia chapa hii imeshuhudiwa kunyakua tuzo mbalimbali za dhahabu kama ya Monde Section kwenye mashindano yaliyofanyika mjini Bordeaux, nchini Ufaransa mwaka 2014.
Bia ya KIBO GOLD sasa inarejea ikiwa na mwonekano maridadi kwa kutengenezwa kwa ubora usio na kifani – ikiwa na viungo vya asilia na kutokuwa na sukari ya ziada na kwa bei ya 1,500/- tu.
Akizungumza katika uzinduzi wa bia hio mwanzoni mwa wiki hii mjini Moshi, Meneja Uvumbuzi wa SBL, Bertha Vedastus, alisema, ‘Kama SBL tunalenga kupanua wigo wetu wa bidhaa kuhakikisha tunakidhi mahitaji ya wateja wetu popote walipo. Na kama tunavyojua Watanzania tunathamini sana urithi na utamaduni katika kila jambo tunalolifanya. Hivyobasi, tunapotafuta maendeleo katika maisha yetu ya kila siku, ni muhimu kuhifadhi na kuthamini urithi na utamaduni wetu. Na kwayo, uwepo wetu wa muda mrefu katika kanda ya Kaskazini umetufanya kuja na maamuzi ya kina ya kudumisha urithi na ufahari wa kanda hii kupitia bia ya KIBO GOLD'.
Bertha aliendelea kuelezea kuwa bia ya KIBO GOLD ina utajiri wa kihistoria na urithi wa ubora ambao kila mtanzania inabidi ajivunie kuuendeleza. Alinukuliwa, ‘ni bia yetu, ya watu wetu na urithi wetu. Tunaamini KIBO GOLD - Kilele Cha Ubora, itaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wapenda bia katika kanda hii nzima’’.
SBL baada ya kutambua mara moja uwezo na thamani ya chapa hiyo ya KIBO GOLD imedhamiria kuirejesha katika mioyo ya wapendwa wa bia kote Ukanda wa Kaskazini. Bia hii yenye sura mpya ya kisasa kwa bia itaongeza mvuto wake kwa soko la ndani na la nje.
About SBL:
Incorporated in 1988 as Associated Breweries, SBL is the second largest beer company in Tanzania, with its beer brands accounting for over 25% of the market by volume.
SBL has three operating plants in Dar es Salaam, Mwanza and Moshi.
Since the creation of SBL in 2002, the business has grown its portfolio of brands year on year. The majority stake acquisition by EABL/Diageo in 2010 has seen increased investment in international quality standards leading to greater job opportunities for the people of Tanzania.
SBL Brands have been receiving multiple international awards and include Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout and Senator. The company is also home to world’s renowned spirits such as Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum and Baileys Irish Cream.
For further information contact;
Rispa Hatibu
SBL Corporate Relations Manager
Tel: 0685 260 901
Email: RISPA.HATIBU@diageo.com
No comments:
Post a Comment