| Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bi. Vivienne Penessis (katikati), na Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Athumani Mlinga (wa pili kulia) kutoka Vodacom Tanzania Plc, wakikabidhi baadhi ya msaada wa vitabu pamoja na vifaa vinginevyo vya shule kwa Mwasisi na Mwanzilishi wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Kiwalani, Mchungaji Elias Mwakalukwa (wa kwanza kushoto) na mwanafunzi wa shule ya kituoni hapo, Cecilia Teotimo (wa pili kushoto) wakati Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwalani, Bi. Lucresia Francis Shayo (wa kwanza kulia) akishuhudia tukio hilo. Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama vile vitabu, madawati, meza, viti, vitanda, magodoro, na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 ikiwa ni jitihada za kuisadia jamii mwishoni mwa wiki. |
No comments:
Post a Comment