Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 19 April 2023

VODACOM YAZINDUA PROGRAMU MAALUM YA TUZO KWA MAWAKALA WA MAUZO, KUWAPELEKA AFRIKA KUSINI

Mkuu wa Idara ya Uwezeshaji wa Kibiashara (HOD Commercial Acquisition) wa Vodacom Tanzania Plc, Grace Chambua akizungumza na mawakala wa mauzo (hawapo pichani) wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa programu maalum ya tuzo kwa mawakala hao ikiwemo kujishindia safari ya kwenda Afrika ya Kusini. Uzinduzi huo ni sehemu ya kampeni mpya inayojulikana kama ‘Zaidi ya Mtandao’ uliofanyika jijini Dar es Salaam na mikoa mingine nchini kote.

Mawakala wa mauzo wa Vodacom Tanzania kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa programu maalum ya tuzo kwa mawakala wa mauzo ikiwemo kujishindia safari ya kwenda Afrika ya Kusini. Uzinduzi huo ni sehemu ya kampeni mpya inayojulikana kama ‘Zaidi ya Mtandao’ uliofanyika jijini Dar es Salaam na mikoa mingine nchini kote.

Dar es Salaam – Aprili 13, 2023: Kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua programu maalumu ya tuzo kwa mawakala wa usajili (freelancers) ambapo programu hii kabambe itawazawadia mawakala wake bora zawadi kemkem ikiwemo safari ya kwenda nchini Afrika Kusini mwisho wa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania Plc, Bi. Linda Riwa amesema kuwa, kwa kutambua mchango mkubwa wa mawakala wake na katika kuwajengea ari ya kufanya kazi kwa bidii, wameamua kuja na programu ya tuzo mahususi kwa ajili yao itakayowawezesha kujinyakulia zawadi mbali mbali kadri wanavyozidi kufanya vizuri katika utendaji wao.

“Tunajivunia kuendelea kuwa kampuni bora ya teknolojia na mawasiliano kupitia ubunifu wa kidigitali unaonufaisha jamii ya Watanzania nchini kote. Leo tunapenda kutambulisha programu yetu mpya ijulikanayo kama "Vodacom Stars" inayolenga kuwanufaisha mawakala wetu wa usajili, ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kwa kuwa wanafamilia wa Vodacom na vile vile kuwawezesha kiuchumi kwani Vodacom ni zaidi ya mtandao,” alisema Bi Riwa.

Bi Riwa alitangaza kuwa kupitia programu hii mpya kwa ajili ya mawakala wa usajili (freelancers) hapa nchini, mawakala watajipatia fursa ya kujishindia zawadi kemkem ikiwemo safari ya kwenda nchini Afrika ya Kusini itakayogharamiwa kila kitu na Vodacom Tanzania. Zawadi nyingine ni pamoja na pikipiki, baiskeli, spika za muziki, bima ya afya, majiko ya gesi ya kupikia, luninga, simu za mkononi na magodoro.

Ili kujiongezea fursa ya kushinda zawadi hizi itawabidi kuonyesha bidii kwa kuwasajili wateja wapya wengi zaidi kujiunga na Mtandao Supa wa Vodacom.

Kwa kumalizia Mkurugenzi huyo wa Biashara aliongezea kuwa pamoja na kujishindia safari na zawadi nyingine, mawakala hao wa usajili wataendelea kupata bonus tofauti tofauti kama fedha taslimu na bando la papo hapo kila wanapofikia malengo ya siku, punguzo la bei za starterpack pamoja bonus ya M-Pesa papo hapo pale mteja mpya aliyeunganishwa atakaponunua bando kwa kutumia M-Pesa. Zawadi na bonus zote zina thamani ya zaidi ya shilling Bilioni 2.

Mawakala wanaofanya vizuri watakuwa wakitangazwa kwa nyakati tofauti huku wakizawadiwa zawadi nyingine zikiwa ni pamoja na pesa taslimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Kampuni hiyo, Ezekiel Nungwi, aliongeza kuwa, “kuhakikisha kuwa mawakala wetu wa usajili wanawafikia wateja na kuwafikishia habari njema za mtandao wa Vodacom tutakuwa na shughuli mbalimbali katika viunga tofauti vya mikoa mbalimbali nchini. Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na uhamasishaji kupitia magari yenye vipaza sauti, kuwatembelea mawakala na wafanyabiashara, pamoja na kuzungumza na wateja moja kwa moja mitaani ili kuwaelimisha kuhusu huduma na bidhaa zetu na kuwaunganisha ili waweze kunufuaika nazo,” alisema Nungwi.

Wakati wa shughuli hizo wateja watakuwa na fursa ya kukutana na mawakala na kujifunza zaidi kuhusu maboresho ya huduma na bidhaa za kampuni hiyo, pamoja na kuunganishwa na Mtandao Supa Tanzania. Nungwi alichukua fursa hiyo kuwataka wateja wote na Watanzania kwa ujumla kujiandaa kunufaika na yale ambayo Vodacom imewaandalia na pia wasisite kuwasikiliza na kuwafuata mawakala ambao watakuwa mitaa tofauti ili kuwahudumia na pia kuwafikishia habari hii njema.

Kwa upande wake mmoja wa mawakala aliehudhuria uzinduzi wa program ya tuzo mkoani Iringa ndg. Japhet Nyalusi alisema amefarijika sana kuona jinsi mtandao wa Vodacom unavyowajali washirika wake na kuwa anatazamia kuunganisha wateja wapya wengi zaidi ili aweze kujishindia zawadi za siku na zile kubwa za mwezi. Vile vile aliongeza kwamba kwenda nchini Afrika Kusini itakua kama ndoto kwake na anaamini akitia juhudi zaidi ataweza kuibuka mshindi.

No comments:

Post a Comment