Kupitia promosheni hiyo ambayo SBL iliwekeza Tzsh milioni 36, jumla ya washindi 22 wametunukiwa zawadi mbalimbali kwa kipindi cha miezi miwili. Washindi walikuwa kutoka kanda za Ziwa, Kusini na Kaskazini ambako promosheni hiyo ilikuwa ikitekelezwa. Zawadi hizo ni pamoja na simu janja, televisheni, pikipiki na gari kama zawadi kuu.
Kwa upande wake Shamimu Hemedi Mushi aliyejishindia zawadi hiyo baada ya kushiriki kwenye promosheni hiyo alisema, “Nimefurahi sana kuibuka mshindi wa gari jipya kabisa baada ya kushiriki Kapu la Wana, Pilsner ni bia ya chaguo langu lakini sikutarajia kushinda zawadi hii kubwa. Naishukuru SBL kwa kuunda promosheni hii na kunizawadia zawadi hii ambayo itabadilisha maisha yangu kabisa.”
Hafla ya makabidhiano hayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa kama Mgeni Rasmi. Mtahengerwa aliipongeza SBL kwa kuandaa promosheni iliyowapa fursa ya kurudisha kidogo kwa jamii, “Naipongeza SBL kwa mpango huu, kupitia promosheni hii SBL imemwezesha mwanamke ambaye leo anaondoka na gari jipya kabisa, ambalo naamini litabadili maisha yake yatakuwa bora kuanzia hapa na kuendelea.”
Kuhusu SBL
Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.
SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza, na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa watu wa Tanzania.
Kampuni za SBL Brands zimekuwa zikipokea tuzo nyingi za kimataifa na ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness stout, na Guinness smooth. Kampuni hiyo pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon's Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don - SBL's maiden local spirit brand na Smirnoff orange.
Kwa maelezo zaidi wasiliana
Rispa Hatibu
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL
Simu: 0685 260 901
Barua pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com
No comments:
Post a Comment