Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 13 March 2023
MSTAHIKI MEYA WA UBUNGO AZITAKA TAASISI KUIGA MFANO WA BENKI YA DCB UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI
Mstahiki Meya wa Ubungo azitaka ya taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB uboreshaji wa elimu nchini.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary Nyaigesha amezitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB katika juhudi zake za uboreshaji wa elimu nchini.
Mstahiki meya aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati akipokea msaada wa madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiluvya, iliyo katika Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam yaliyotolewa na DCB kupitia kampeni yake ya ‘Elimu Mpango Mzima na Mama Samia’.
“Kwa kufanya hivi, Benki ya DCB inaunga mkono juhudi za Rais wetu Mpendwa, Mheshiwa Dk. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watu wake maendeleo katika uboreshaji wa elimu nchini”, alisema mstahiki meya.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bwana Isidori Msaki akizungumza mahali hapo alisema, madawati hayo ni sehemu ya madawati 150 yeye thamani ya shs 37,500,000 wanayoyatoa katika Manispaa tano za jiji la Dar es Salaam ikizingatiwa kuwa wao ndio wanahisa waanzilishi wakati benki ikianzishwa miaka 20 iliyopita.
“Tunajivunia ushirikiano wenye tija na Manispaa hizi kwani kwa kipindi cha miaka 20 kwa mtaji wa shs bilioni 1.7 tuliokuwa nao mwaka 2002, benki imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na imeweza kutoa gawio la jumla ya shs bilioni 11.5 kati ya hizo Manispaa zikipokea gawio la shs bilioni 4.55”, alisema Bwana Msaki.
Mkurugenzi huyo alisema, mafanikio haya yanawezekana chini ya uongozi mahiri wa Bodi ya benki hiyo inaoongozwa na mwanamama shupavu Bi. Zawadia Nanyaro.
“Ni matumaini ya DCB kuwa msaada utazidi kuimarisha mahusiano kwa manufaa ya pande zote mbili, DCB kama mtoa huduma za kibenki na mdau wa maendeleo na kwa manispaa yako kama wadau wetu muhimu”, alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment