Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Raisi, Kazi, Uchumi Na Uwekezaji, Mh. Mudrick Soraga akitoa neno kwenye hafla hiyo akiwa kama Mgeni Rasmi. Benki ya Equity Tanzania imeingia makubaliano ya kufanya kazi na taasisi ya ZEEA pamoja na SMIDA za Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha wanatoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wakubwa na wadogo na kuwapa elimu za kifedha kama sehemu ya mkakati wa Benki kuhakikisha wanatoa huduma bora na gharama nafuu kwa kila Mtanzania.
Makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya ZEEA na SMIDA ambapo Equity kama benki wanakwenda kutoa mikopo bila riba kwa jamii ya wazanzibari, Makubaliano haya yanakwenda kuleta mageuzi makubwa sana katika sekta ya fedha na uchumi kwani yatawezesha taasisi zetu kuleta maendeleo ya haraka kwa vijana, si tu maendeleo bali kukuza elimu ya fedha na ukopaji wenye malengo na tija.
Makubaliano haya yatasaidia katika suala zima la kuongeza ajira kupitia nguzo ya ujasiliamali kwani wajasiliamali watapata mitaji ya kutosha kukuza biashara zao sambamba na kuongeza ubunifu. Ili kufikiwa matamanio haya, Benki ya Equity itakuwa na mengi na mahususi ambayo ni pamoja na;
- Kutumia miundombinu ya kibenki katika kuwezesha utoaji wa mikopo ambayo imethibitika, hii ni pamoja na mifumo na rasilimali watu.
- Kutumia uzoefu wa ufuatiliaji mikopo ili kuhakikisha kuwa pesa inayokopeshwa pasi na riba inarejeshwa kwa wakati na kulingana na vigezo na masharti yaliyokubaliwa.
- Kutoa taarifa kwa vyombo wabia (ZEEA na SMIDA) juu ya ufanisi wa program hii kwa wakati.
- Kutoa mikopo kwa wakati (ndani ya siku 14 za kazi).
- Kuendelea kutoa mikopo bila riba wakati wote program hii kwa wajasiriamali katika Nyanja zote za uzalishaji.
- Kutumia mtaji wake katika kufanikisha program hii ya kukopesha wajasiriamali bila riba.
No comments:
Post a Comment