Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 23 March 2023

DKT. MWIGULU NCHEMBA ATETA NA KAMISHNA WA BIASHARA KANDA YA AFRIKA WA UINGEREZA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi Kamishna wa Biashara Kanda ya Afrika wa Serikali ya Uingereza, Mhe. John Humphley, jarida linaloonesha mafanikio ya miaka miwili madarakani ya Serikali ya Awamu ya Sita, ya Samia Suluhu Hassan, walipokutana kwa mazungumzo ya kikazi katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, jijini London, Uingereza.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wa pili kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Biashara wa Uingereza anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. John Humphley, baada ya kumaliza mazungumzo ya kikazi katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini London, Uingereza. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzaibar, Dkt. Juma Malik Akil, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wa pili kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Biashara wa Uingereza anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. John Humphley (wa pili kulia), baada ya kumaliza mazungumzo ya kikazi katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini London, Uingereza. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt. Asha-Rose Migiro. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzaibar, Dkt. Juma Malik Akil na kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Kamishna wa Biashara Kanda ya Afrika wa Serikali ya Uingereza, Mhe. John Humphley, walipokutana kwa mazungumzo ya kikazi katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, jijini London, Uingereza.

Na Benny Mwaipaja, London

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Tanzania amelishauri Shirika la Kimataifa la Uwekezaji la Uingereza (British International Investment - (BII), kuongeza kiwango cha uwekezaji nchini Tanzania ili kukuza biashara

Dkt. Nchemba ametoa wito huo Jijini London, nchini Uingereza, alipoongoza Ujumbe wa Tanzania uliokutana na Menejimenti ya Shirika hilo, ambalo limewekeza katika baadhi ya miradi nchini hapa.

Alisema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, kilimo, utalii, madini, viwanda na huduma pamoja na rasimali za asili kama vile gesi na maji kwa ajili ya kuzalishaji wa nishati, ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, madini pamoja na hali ya amani nchini, ambavyo kiujumla vinaweka mazingira ya kuvutia kiuwekezaji.

Dkt. Nchemba ameialika timu ya wataalamu kutoka BII kuitembelee Tanzania na kufanya mazungumzo na taasisi na mashirika mbalimbali pamoja na sekta binafsi ili kuangalia maeneo ya kuwekeza kwa faida ya pande zote zinazohusika.

Naye Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, alisema kuwa Zanzibar, ikiwa sehemu ya Tanzania, inatekeleza program ya uchumi wa bluu inayohitaji uungwaji mkono wa Taasisi za fedha za Kimataifa na kuiomba Taasisi hiyo kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Zanzibar

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uingereza la Uwekezaji (BII) Bw. Chris Chijiutomi, aliihakikishia Tanzania kwamba iko tayari kuongeza uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta binafsi ikiwa ni sera ya Serikali ya Uingereza ya misingi ya kuanzishwa kwa Shirika hilo.

Alisema kuwa Shirika lake lina mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 11 lakini imewekeza Tanzania kiasi cha dola za kimarekani milioni 215 pekee hivyo kuitaka Tanzania kuainisha miradi ya kipaumbele ambayo shirika hilo litachambua na kutoa fedha kwa kushirikiana na sekta hiyo binafsi.

No comments:

Post a Comment