Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 9 March 2023

BENKI YA AKIBA WAZINDUA "WARIDI AKAUNTI" KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kidijitali kwa Benki ya Akiba, Bi. Magreth Mwasumbi akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Akaunti maalumu wa kwa ajili ya Wanawake inayoitwa "WARIDI AKAUNTI". Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba, Dora Saria. Uzinduzi huu umembatana na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika hafla ndogo zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba, Dora Saria akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Akaunti maalumu wa kwa ajili ya Wanawake inayoitwa "WARIDI AKAUNTI ". Uzinduzi huu umeambatana na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika hafla ndogo zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo Jijini Dar es salaam.    

Picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa Huduma mpya ya AKAUNTI YA WARIDI ya wafanyazi wanawake wa Akiba Commercial Bank Plc katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Machi 08, 2023 katika ofisi za makao makuu jijini Dar es Salaam.


Picha mbalimbali za matukio ya wafanyazi wanawake wa Akiba Commercial Bank Plc katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Machi 08, 2023 katika ofisi za makao makuu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment