Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 23 January 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA CEMENT UJENZI WA KITUO CHA POLISI KIBURUGWA

Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala, Edward Mwoleka (kushoto), akikakabidhi msaada wa mifuko 100 ya cement kwa Diwani wa kata ya Kiburugwa, Mh. Fatuma Michael iliyotolewa na Benki ya Tanzania Commercial Bank kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi cha kata hiyo ikiwa ni utamaduni wa Benki hiyo kujitolea katika kusaidia jamii. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta na Afisa wa TCB, Adam Lameck.

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Gloria Mutta (kulia) akikakabidhi msaada wa mifuko 100 ya cement kwa Diwani wa kata ya Kiburugwa, Mh. Fatuma Michael iliyotolewa na Benki ya Tanzania Commercial Bank kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi cha kata hiyo ikiwa ni utamaduni wa Benki hiyo kujitolea katika kusaidia jamii. Wengine pichani ni Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala - Edward Mwoleka, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Betha Minga, Afisa wa TCB - Adam Lameck pamoja na Diwani wa kata ya Charambe.

Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala, Edward Mwoleka (kulia), akikakabidhi msaada wa mifuko 100 ya cement kwa Mtendaji Kata wa Kiburugwa, Mustapha Nguyu iliyotolewa na Benki ya Tanzania Commercial bank kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi cha Kata hiyo ikiwa ni utamaduni wa Benki hiyo kujitolea katika kusaidia jamii. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment