Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) - Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la benki hiyo lililozinduliwa katika Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaam. Tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma ya kifedha muda wote. Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) - Gloria Mutta, Mkurugenzi wa Masoko - Deo Kwiyukwa, Meneja wa TCB Tawi la TPA - Anastela Kabudi, Mkurugenzi wa Sheria - Mystica Mapunda Mkurugenzi wa Hazina wa TCB - Wenceslaus Fungamtama.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) - Sabasaba Moshingi (kushoto), akifungua kisanduku maalum kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la benki hiyo lililozinduliwa katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaama. Tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24 ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma za kifedha muda wote. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko wa benki hiyo - Deo Kwiyuka, pamoja na Meneja wa TCB Tawi la TPA - Anastela Kabudi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) - Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) lililopo posta jijini Dar es Salaam. Tawi hilo litakuwa likifanya kazi masaa 24.
Meneja Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la TPA - Anastela Kabudi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa leo.
No comments:
Post a Comment