Meneja Habari na Uhusiano NHC, Muungano Saguya akifafanua jambo kwa Wanahabari (hawapo pichani) katika mkutano huo. |
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara NHC, William Genya katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika jengo la NHC Kambarage House jijini Dar es Salaam.
Genya amesema kuwa Sera hiyo ina lenga kuwapa fursa wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini, ambapo Sera hiyo itaenda kufungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ili kuunga mkono maono na maelekezo ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binfasi ambayo ni injini ya kuleta maendeleo ili iwekeze mitaji yao katika kujenga uchumi wa Taifa Letu.
“Uzinduzi huo wenye lengo la kuwaalika Watanzania kushiriki kwenye Sera hiyo iliyoanzishwa na Shirika tangu mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika. Maboresho ya mwisho yalifanyika mwaka 2022 na yamezingatia kuvutia Uwekezaji kwa kuwa yana maslahi kwa Shirika la Uwekezaji” Alisema Genya.
Ameongeza kusema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu huu jumla ya miradi mia moja kumi na moja (111) ilitekelezwa ikiwa na thamani ya TZS Bilioni 300. Katika miradi hiyo, miradi 81 yenye thamani ya shilingi Bilioni 240 imekamilika na kuanza kutumika na miradi 30 yenye thamani ya TZS Bilioni 60 inaendelea kukamilishwa.
Amebainisha kuwa miradi hiyo imechangia upatikanaji wa ajira, kuboresha mandhari ya miji yetu, kuongeza mapato ya Shirika, kuongeza wigo wa kodi za Serikali, kuongeza maeneo kwa ajili ya biashara na makazi na kuipanga miji yetu.
“Katika uzinduzi huo mkubwa tunakusudia kuwa na washiriki takribani 600 kutoka tasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, vyama na bodi za kitaalum pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi ambao wamealikwa. Mabalozi wa nchi zenye wawekezaji wakubwa wamealikwa na wawakilishi wa Kamati za Bunge zinazogusa shughuli za NHC.
Amesisitiza kuwa pamoja na mialiko mbalimbali iliyotolewa pia kwa wale wanaohitaji kushiriki katika uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 21 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam wanaweza kupiga simu kwa nambari +255 767 566 299 au +0658 662 800 au kutuma ujumbe kupitia baruapepe nhcjv@nhc.co.tz
No comments:
Post a Comment