Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 24 October 2022

BENKI YA NBC ILIVYOIPAMBA DERBY YA KARIAKOO

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kulia) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa klabu ya Yanga, Feisal Salum alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi mililioni 1 kwa mchezaji wa klabu ya Yanga, Feisal Salum alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kushoto) akisalimiana na wapenzi wa mchezo huo wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Brendansia Kileo (katikati) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.
“Tumetumia mechi hii kubwa kuwakaribisha wateja wetu wa tawi letu jipya lililopo wilayani Kigamboni lengo likiwa ni kufurahi nao katika ligi hii. Zaidi ya wateja 70 wilayani humo walipata fursa ya kutazama mechi hiyo kwa udhamini wa benki ya NBC ambapo tuliweza kuwapatia usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi majumbani mwao wakiwa salama kabisa,’’ – David Kigwile, Kaimu Mkuu wa Idara ya Masoko, Benki ya NBC.
Mbali na kutoa fursa kwa wapenzi wa soka kufuatilia mechi hiyo kupitia screen kubwa pia walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wa benki hiyo waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo pamoja na viunga vya uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.


Dar es Salaam, Octoba 24, 2022 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana iliipamba mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga na Simba kwa kuandaa matukio kadhaa kwa ajili ya wapenzi wa mchezo huo ikiwemo wateja wake wakubwa na wadogo sambamba na kukabidhi tuzo na zawadi kwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba.

Shughuli zote hizo ziliongozwa na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi ambae alipata wasaa wa kukabidhi tuzo na zawadi ya fedha kiasi cha sh mil 1, kwa mchezaji wa klabu ya Yanga, Feisal Salum alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na maelfu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, lilitanguliwa na matukio mengine ambapo benki hiyo iliandaa mwaliko rasmi kwa ajili ya wateja wake wakubwa zaidi ya 50 waliopata wasaa kupata chakula cha mchana pamoja na viongozi wa benki ya NBC kisha kwa pamoja walielekea Uwanja wa Taifa kushudia mechi hiyo wakiwa katika msafara maalum.

Akizungumzia hatua ya benki hiyo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo, David Kigwile alisema mbali na wateja wakubwa, benki hiyo pia ilitoa tiketi 70 kwa ajili ya wateja wake wadogo wa tawi jipya la Kigamboni ili waweze kwenda kutazama mtanange huo ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha waweze kufurahia huduma za benki hiyo wilayani humo.

“Tumetumia mechi hii kubwa kuwakaribisha wateja wetu wa tawi letu jipya lililopo wilayani Kigamboni lengo likiwa ni kufurahi nao katika mchezo huu pendwa. Zaidi ya wateja 70 wilayani humo walipata fursa ya kutazama mechi hiyo kwa udhamini wa benki ya NBC ambapo tuliweza kuwakatia tiketi wote pamoja na kuwapatia usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi majumbani mwao wakiwa salama kabisa,’’ alisema.

Aidha, benki hiyo iliandaa ‘Screen’ kubwa kwenye baadhi ya maeneo wilayani humo ili kutoa fursa kwa wapenzi wa mchezo huo ambao hawakuweza kufika uwanjani ili waweze kufurahia mechi hiyo.

“Mbali na kutoa fursa kwa wapenzi wa soka kufuatilia mechi hiyo kupitia screen kubwa pia walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wetu waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo pamoja na viunga vya vya uwanja wa Benjamin Mkapa.’’ Alisema.

No comments:

Post a Comment