Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KANU EQUIPMENTS, Warren Heger (kulia) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya kutoa mikopo nafuu kwa wakulima kwa ajili ya kununulia pembejeo za kilimo ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya kilimo nchini.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwakushirikiana na KANU EQUIPMENT jana wametia saini mkataba wa maridhiano ili kutoa mikopo nafuu kwa wakulima kwa ajili ya kununulia pembejo za kilimo ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya NBC, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Elvis Nduguru alisema; “Sisi Benki ya NBC tukiwa wadau wakubwa wa kilimo nchini tunathamini na kutambua mchango wa kilimo katika pato la taifa. Kilimo kinachangia zaidi ya asilimia 65% ya uzalishaji nchini na pia kinatoa zaidi asilimia 75% ya ajira zote. Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu.
Hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Kilimo imetangaza mpango maalum wa kuboresha kilimo ujulikanao kama “ajenda 10/30” ambao unalenga kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilia 5 mpaka 10 ifikapo mwaka 2030. Sisi Benki ya NBC tukiwa wadau wakubwa wa kilimo nchini, tumeona ni vema kuunga mkono juhudi hizi za Serkali yetu kwa kukutana na wenzetu wa KANU, ambao ni watalaam katika masuala ya uuzaji wa vifaa vya kilimo kutoa mikopo nafuu ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji.
Kupitia maridhiano haya, wanunuzi wa pembejeo za kilimo kupitia kampuni ya KANU nchi nzima, ikiwemo matrekta, wataweza kupata mikopo nafuu na ya haraka kununua vifaa kama matrekta ndani ya siku kumi na nne” alisema.
Awali Mkuu wa Kitengo cha Kilimo wa Benki hiyo Raymond Urassa akifafanua kuhusu faida na vigezo kwa wakulima kupitia bidhaa hii alisema; “makubaliano haya tunayosaini leo yatawawezesha wakulima na wafanyabiashara waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, kupata zana za kilimo na pembejeo kwa gharama nafuu na kwa wakati stahiki.
Awali Mkuu wa Kitengo cha Kilimo wa Benki hiyo Raymond Urassa akifafanua kuhusu faida na vigezo kwa wakulima kupitia bidhaa hii alisema; “makubaliano haya tunayosaini leo yatawawezesha wakulima na wafanyabiashara waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, kupata zana za kilimo na pembejeo kwa gharama nafuu na kwa wakati stahiki.
Lengo letu ni kuhakikisha Mkulima anapata trekta lake ndani ya siku kumi na nne huku wakiwa na muda rafiki wa marejesho ya mkopo kulingana na msimu wa zao husika” alisema. Mwakilishi wa KANU EQUIPMENT Edson Nalogwa alieleza furaha waliokuwa nayo kusaini na kutoa huduma kwa wakulima kupitia Benki ya NBC akisema; Benki ya NBC ni sehemu sahihi katika ukuzaji wa kilimo nchini ikiwa wana bidhaa mbali mbali za kusaidia kukuza Kilimo.
Mikopo hii ni rafiki na ina masharti nafuu, ikiwamo chombo chenyewe kutumika kama dhamana ya mkopo” alisema. Benki ya NBC ni mdau wakubwa wa kilimo nchini ikitoa mikopo mingi kwenye sekta ya kilimo na mnyororo mzima wa sekta hiyo yenye kuajiri watu wengi zaidi nchini.
No comments:
Post a Comment