Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 12 August 2022

NHC YAONGOZA KIKAO CHA UANZISHWAJI UMOJA WA WAENDELEZAJI MILIKI NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu (wa kwanza kushoto) akichangia katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Fedha kutoka TMRC Bw. Oswald Urassa (aliyenyoosha mkono) akichangia katika kikao hicho.
Viongozi hao wakiwa katika majadiliano.
Picha ya pamoja ya viongozi kutoka Taasisi mbalimbali walioshirikia katika kikao hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa - NHC Nehemiah Mchechu kwa kushirikiana na wadau wengine wa Sekta ya Miliki wameanza mchakato wa kuanzisha Umoja wa Waendelezaji Miliki nchini.

Mchakato huo umeanza leo kwa majadiliano ya awali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ghorofa ya 8 Kambarage House NHC DSM kwa lengo la kuangalia namna ya kuanzisha Umoja huo ambao utakuwa ni chombo cha kuwaunganisha wadau wa Sekta ya Miliki nchini.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu amesema kuwa mchakato huo ambao ulianza tangu mwaka 2015 lakini kutokana na sababu mbalimbali ukashindwa kuendelea, sasa umefika wakati wa kuwa na chombo muhimu katika Sekta ya Miliki nchini.

“Hapo awali kulikuwa na wazo la kuanzishwa kwa umoja huu lakini baadaye ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali sasa anaona umefika wakati muafaka wa kuona kwa pamoja tunawezaje kuanzisha umoja wetu ambao utatusaidia kuzungumza kwa pamoja juu ya fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hii lakini pia kuzitangaza fursa hizo ili kuleta tija kwa umoja na Serikali kwa ujumla” Alisema Mchechu.

Ameongeza kusema kwamba kupitia umoja huo pamoja na mambo mengine wanachama watapata nafasi ya kushauriana, kushirikishana na kutangaza masuala mbalimbali ya Sekta ya Miliki ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Morgage Refinance Company Limited - TMRC Oscar Mgaya amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kuwa na umoja huo ambao utawaunganisha waendelezaji miliki wote ili kuweza kutumia fursa zilizopo.

Ameongeza kusema kuwa kuanzishwa kwa umoja huo ambao utakuwa ni wa kudumu utaweza kuwaunganisha wadau katika sekta hiyo ili kwa pamoja watumie vyema fursa zitakazojitokeza ili kuleta tija kwa wadau hao na Serikali kwa ujumla.

Majadiliano hayo yameziusisha Taasisi mbalimbali ikiwemo NHC, PSSSF, NSSF, Watumishi Housing na TMRC.

No comments:

Post a Comment