Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 9 August 2022

MAINSTREAM MEDIA LIMITED WAENDESHA MAFUNZO MAALUMU KWA WAKUFUNZI WA VICOBA

 Mkurugenzi wa Mifumo ya kifedha na Ubunifu wa kampuni ya Mainstream Media limited Bw. Deogratius Mosha akiendesha mafunzo kwa Wakufunzi wa Vicoba wakati wa uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu, Kampuni ya Mainstream Media Limited na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam.
 
Wakufunzi wa Vicoba wakifuatilia kwa makini Mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu , Kampuni ya Mainstream Media Limited na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam. Mmoja wa Wakufunzi wa Vicoba akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu , Kampuni ya Mainstream Media Limited na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam.Mmoja wa Wakufunzi wa Vicoba akikabidhiwa cheti cha a kushiriki wakati wa uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu, Kampuni ya Mainstream Media Limited na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam. Mzee, Sulum Sultan, Ambaye ni mmoja kati ya walezi wa Vicoba kutokea Kampuni ya Rasuki ambaye pia ni muasisi wa ubunifu akifafanua jambo kwa washirki wa Mafunzo walioshiriki uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu , Kampuni ya Mainstream Media Limited (https://mainstreammedia.co.tz ) na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa HumTech Bw. Alfred Rukatila akiendesha mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu, Kampuni ya Mainstream Media Limited (https://mainstreammedia.co.tz ) na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam. Picha ya pamoja kwa washiriki wa Mafunzo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo wezeshi kwaajili ya matumizi ya mfumo wa kidijitali katika usimamizi wa usimamizi wa vikundi vya vicoba hapa nchini Tanzania . Mafunzo haya yameendeshwa na waandaaji wa mfumo huu , Kampuni ya Mainstream Media Limited (https://mainstreammedia.co.tz ) na Kuhudhuriwa na wakufunzi wa vikundi vya Vicoba hapa Mjini Dar es Salaam.
Ni Katika hoteli ya Sesshels – Millenium towers ambapo mafunzo haya yame fanyika yakikutanishawakufunzi wa vikundi vya Vicoba takribani 30 kutoka maendeo Mbalimbali ya mji wa Dar es Salaam. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wakufunzi juu ya uhimu wa mifumo ya kiteknolojia katika kutunza taarifa za kifedha na pia umuhimu wa ushiriki katika mabadiliko ya kiteknolojia yanayoleta tija na ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za vikundi hivi. 
Akizungumza kwenye Mafunzo haya Mzee, Sulum Sultan, mmoja kati ya walezi wa Vicoba kutokea Kampuni ya Rasuki ambaye pia ni muasisi wa ubunifu huu ameeleza kwamba kutokana na kasi ya mabadiliko ya Tehama na changamoto zinazowakabili wanavicob, alilazimika kuwatafuta wataalamu wa Tehama ili waweze kuja na suluhisho la uendeshaji wa vikundi hivi, “Miaka ile ya zamani mabenki yalikuwa yanatumia vitabu kutunza taarifa ila siku hizi wanatumia tu simu zao za mkononi, Niliwaza na kuona kwanini na sisi wana Vicoba tusiwe na mifumo ya simu?”. Na ndipo kazi hii ambayo leo inahitimishwa kwa mafunzo wezeshi ilipoanzia ya kuunda mfumo wa Vicoba Poa.
 
Pamoja na haya, pia Mkurugenzi wa Mifumo ya kifedha na Ubunifu wa kampuni ya Mainstream Media limited Bw. Deogratius Mosha amebainisha kuwa Mageuzi ya kiteknolojia kwenye uendeshaji wa huduma za kifedha hapa nchini na duniani kote hayaepukiki, amegusia kuwa kwa Pamoja Kampuni ya Mainstream Media imeshirikiana na kampuni ya HumTechnologies ili kukamilisha uvumbuzi wa mfumo huu ambao unakwenda kuleta mageuzi makubwa na kuongeza ufanisi na uwazi katika uendeshaji shughuli za Vicoba hapa nchini. Utawezesha wanavicoba kusimamia na kushiriki shughuli za vicoba kwa kutumia simu popote walipo duniani.

Naye Mkurugenzi wa HumTech Bw. Alfred Rukatila ametumia mafunzo haya kuwaomba wakufunzi hawa kueneza ujumbe kote Tanzania kuwa Teknolojia imepanuka sana na inakua kwa kasi hivyo wasikubali kubaki nyuma na watumie fursa hizi na bunifu hizi kusonga mbele Zaidi. Ubunifu huu ni matunda ya vijana wa Kitanzania.

Msimamizi wa kitengo cha Biashara na bidhaa hii wa Mainstream Media, Bi, Diana Steven amefananua wazi kwamba Mfumo ambao umetengenezwa unaitwa Vicoba Poa na unawezesha wanachama wa Vicoba kuziona na kutunza taarifa zao kwa kutumia simu zao za kiganjani. Amegusia kwamba Mfumo huu umezingatia unyeti wa taarifa za fedha na hautoruhusu mtu ambaye sio mhusika kuona taarifa za kikundi. Mambo ambayo yamezingatiwa ni Pamoja na kununua hisa kiganjani, kuomba mkopo kwa simu, kupiga kura kwenye mambo mbali mbali Pamoja na kupata taarifa za michango, marejesho na vikao bwa kutumia simu. Ametoa rai kwa wanavicoba rasmi na wale wasio rasmi (wenye vikundi vya kuweka na kukopa au ujirani mwema) kuanza kutumia mfumo huu ili kuleta urahisi wa uendeshaji shuhuli zao, Mfumo unafikika kupitia tovuti ya www.vicobapoa.co.tz au kwa mawasiliano 0677 77 44
Moja kati ya malengo yaliyoanishwa katika mafunzo haya ni Pamoja na mkakati wa kuendelea kutoa elimu kwa vikundi na wakufunzi wa Vicoba pote nchini ili kuweza kuongeza chachu na hamasa ya matumizi ya Tehama katika kuleta Maendeleo ya Nchi yetu ya Tanzania. 
Katika mafunzo haya Mmoja kati ya wakufunzi walio hudhuria Bi. Veronica Mlele Kutoka UPENDO VICOBA, Amesema anamshukuru Mungu kwa kusikia kilio chao cha Muda mrefu kwani moja ya changamoto wanayopata sasa ni wanachama kutokuwa na muda wa kushiriki vikao, na wakati mwingine kukosa taarifa sahihi za uendeshaji wa vikao na makusanyo, Jambo ambalo hupelekea vikundi vingi kufa, Ila kwa hatua hii anaishukuru mfumo huu wa vicoba Poa na anaaamini utapunguza changamoto hii ya usimamizi wa vicoba
Mafunzo haya maalumu yamekutanisha Wakufunzi mbalimbali wa Vicoba kutoka kampuni za Rasuki, smart ways, Zakale Foundation, C.P.O, LTI, CHAKIWAMU GROUP – KIPAWA na Agriculture Group.
Baada ya mafunzo haya washiriki wote walipatiwa vyeti maalumu kama ishara ya kufuzu mafunzo maalumu ya matumizi ya Mfumo huu wa Tehama katika usimamizi wa Vicoba Nchini Tanzania ulioandaliwa na Kampuni ya Mainstream Media Limited

Imetolewa na
Diana Steven
Meneja Biashara na Bidhaaa – Mainstream Media Limited
Diana.steven@mainstreammedia.co.tz

No comments:

Post a Comment