Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika, Mhandisi Ridhiwani Mringo akitambulisha baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurungezi wa Benki kwa Mgeni Rasmi, Spika wa Bunge Mh. Dk Tulia Ackson alipowasili wakati wa Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara. Hafla hii ilifanyika Ijumaa Tarehe 19 Agost 2022, Makao makuu ya Benki Kijitonyama, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mwanga Hakika, Bwana, Jagjit Singh, akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara. Hafla hii ilifanyika Ijumaa Tarehe 19 Agost 2022, Makao makuu ya Benki Kijitonyama, Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Godwin Gondwe akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara.
Mgeni Rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara.
Mgeni Rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akizindua rasmi Muonekano mpya wa Bneki ya Mwanga kwenye Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara.
Mgeni Rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akiwa Katika picha ya Pamoja na wajumbe wa bodi wakati wa Uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara.
Mgeni Rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahisa mara baada ya uzinduzi wa Benki ya Mwanga Hakika kuwa Benki ya Biashara.
Dar es Salaam - Benki ya Mwanga Hakika yawa benki ya biashara. Ambapo awali benki hii ilikuwa benki ya mitaji midogo na ukuaji huu utawapa wateja wao fursa ya kupata huduma nyingi zaidi ya zile walizokuwa wakipata awali. Mapinduzi ya tehama yamewezesha benki Mwanga Hakika kuwa benki ya biashara na yenye ushindani kwenye soko, sambamba na hilo wingi wa wateja na ongezeko la mtaji ni baadhi ya sababu zilizofanya benki hii kupanua wigo wake na kuwa benki ya biashara kwa lengo la kuwahakikishia wateja wao usalama,urahisi na ukaribu wa huduma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika, Mhandisi Ridhiwani Mringo amesema kuwa, lengo kuu ni kupanua wigo wa kibiashara ili kufikia malengo ya kuwa benki kubwa ndani na nje ya Tanzania.Pamoja na hayo benki ina lengo la kuimarisha ukaribu na wateja wake na kuhakikisha wanapata huduma bora na nafuu.
Alisema kuwa, benki ya Mwanga Hakika inaonekana changa lakini ina historia ya zaidi ya miaka ishirini (20) katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wateja wake kupitia benki shiriki ya Mwanga Community Bank iliyokuwa ikijulikana kama “Benki ya Wananchi Mwanga”,ambayo ilianzishwa mwaka 2000.. Pia alisema kuwa Benki ya Mwanga Hakika imekuwa kwa kiasi kikubwa sana na tukio hili ni la kihistoria ambapo miaka miwili nyuma (tarehe 15 Agosti, 2020) benki tatu ziliungana ambazo ni (EFC Tanzania Microfinance Bank, Hakika Microfinance Bank na Mwanga Community Bank) zilipounganishwa na kuunda benki mpya iliyojulikana kama, Mwanga Hakika Microfinance Bank Limited (MHB).
Na Agosti mwaka huu, imefanikiwa kuwa benki ya kamili ya kibiashara. Pia alisema kuwa,muungano huo haukuwa wa kihistoria tu bali ulikuwa na changamoto, kwani kulikuwa na >benki tatu tofauti, >miundo mitatu tofauti ya uongozi, >mifumo mitatu tofauti ya uendeshaji, >tamaduni tatu tofauti wa kufanya kazi, na makundi matatu tofauti ya Wanahisa,lakini bado tulipata msingi wa pamoja wa kuungana na kuunda benki moja kwa maslahi ya wadau wake wote. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mwanga Hakika,Bwana, Jagjit Singh, alisema kuwa “Ukubwa wa sasa wa Mizania ya benki ya Mwanga Hakika (Total Assets) ni Bilioni 111, -Mikopo ya thamani ya Tsh. Bilioni 72, Amana za Wateja (Customer Deposits), ni Tsh. Bilioni 71, Uwiano wa Mikopo isiyolipika (Non-Performing Loans Ratio) ni 5.49% tu, Idadi ya Wafanyakazi ni 106, na Idadi ya Matawi ni 7 ambayo ni (Kijitonyama - Dar es Salaam, Tegeta - Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanga na Same).
Aliongeza kuwa, benki ya Mwanga Hakika imekuwa benki ya biashara sasa ambapo wateja wake wategemee huduma nyingi zaidi ya zile zilizokuwa zikitolewa awali.Sambamba na hayo, benki hiyo inategemea kutanua utoaji wa huduma zao kwenye baadhi ya sekta kama vile, sekta ya kilimo, biashara, na madini. Ambapo pia itaimarisha uhusiano wao uliopo na Wakandarasi wengi hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi”.
No comments:
Post a Comment