Picha ya pamoja kati ya meza kuu na baadhi ya wanufaika wa programu ya Kilimo Viwanda (wamesimama kwa nyuma) kwenye hafla hio ya kuwatunuku vyeti vya utambulisho. |
Wanufaika wa programu ya ufadhili wa masomo, Kilimo Viwanda kwenye picha ya pamoja wakiwa wameshikilia vyeti vyao vya utambulisho wa ufadhili huo. |
Picha ya pamoja ikijumuisha wafanyakazi wa SBL, uongozi wa chuo cha Kilacha na wanafunzi wa chuo hicho cha kilimo ambao ni wanufaika wa programu ya Kilimo Viwanda. |
Kwa mujibu wa SBL, wamedhamiria kuwaandaa wanafunzi wa vyuo kujiajiri wenyewe katika fani ya kilimo baada ya kuhitimu kozi zao za stashahada ikiwa pia miongoni mwa nguzo zao za kujenga jamii endelevu ifikapo mwaka 2030 kupitia fursa sawa na jumuishi za elimu, ujuzi, rasilimali ili kujenga jumuiya shirikishi ambapo kila mtu atanufaika.
Katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya utambulisho waliopata ufadhili huo katika taasisi ya mafunzo ya kilimo Kilacha. Alice Kilembe, meneja wa kiwanda cha Moshi, alisema, 'SBL inajivunia kuwa na historia ya kuimarisha sekta ya kilimo; tunafanya kazi na mamia ya wakulima nchini Tanzania ambao wao hutuuzia nafaka za kutengeneza bia kama vile mahindi, mtama na shayiri; kwa sababu hiyo, programu hii imeundwa ili kuwatayarisha wanafunzi kuwa wakulima wakubwa na wenye mafanikio katika kilimo biashara'.
"Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, programu yetu ya kilimo pia imetoa msaada wa kiufundi na kifedha ambao umechangia maendeleo ya wakulima 400 na jamii zinazowazunguka, na tumeweza kukusanya malighafi hadi tani 18,000 kila mwaka, hivyo kukuza kipato cha wakulima na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia ulipaji kodi wa mara kwa mara', alisisitiza.
SBL imeahidi kuendeleza mchango wake kuimarisha kilimo nchini kwa kuanza na vijana vyuoni kupitia mpango wao wa ufadhili wa masomo ujulikanao kama Kilimo Viwanda Scholarship, ambao tayari zaidi ya wanafunzi 200 wamenufaika tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2019.
Mkuu wa chuo hicho Benito Mwenda alipongeza juhudi za SBL katika kuwaelimisha wanafunzi kuhusu ulimwengu wa kilimo cha biashara. Mkuu huyo wa shule alionekana kujiridhisha kuwa mpango huo tayari umeanza kuweka msingi imara kwa wanafunzi akisema, ‘chuo kinapenda kuwashukuru vya kutosha kwa dhamira yenu SBL ya kuwasaidia wanafunzi hawa hata baada ya kumaliza masomo yao, naweza kusema SBL mmekuwa mfano wa kuigwa hapa nchini katika kuwekeza kwenye kilimo kupitia wanafunzi waliopo vyuoni. Hivyo basi, natumai makampuni mengine yatajifunza kutoka kwenu'. Alihitimisha.
About SBL:
Incorporated in 1988 as Associated Breweries, SBL is the second largest beer company in Tanzania, with its beer brands accounting for over 25% of the market by volume.
SBL has three operating plants in Dar es Salaam, Mwanza and Moshi.
Since the creation of SBL in 2002, the business has grown its portfolio of brands year on year. The majority stake acquisition by EABL/Diageo in 2010 has seen increased investment in international quality standards leading to greater job opportunities for the people of Tanzania.
SBL Brands have been receiving multiple international awards and include Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout and Senator. The company is also home to world's renowned spirits such as Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon's Gin, Captain Morgan Rum and Baileys Irish Cream.
About WaterAid Tanzania
Since 1983, WaterAid Tanzania (WAT) has contributed to increasing access to water, sanitation, and hygiene (WASH) services, working closely with the Government, Civil Society Organizations, and other International NGOs. WaterAid Tanzania has delivered basic water and sanitation services to communities with the vision of reaching everyone everywhere. The organization promotes sustainable services in the country, integrate WASH with other areas of development at sub-national to the national level, address inequalities in accessing WASH services in the country, and improve positive hygiene behaviours. To date, WaterAid has reached more than 8 million Tanzanians across 11 regions of both the mainland and Zanzibar with access to WASH services. WaterAid intends to continue extending its role in Tanzania through working collaboratively and in partnership with others to drive transformational change
For further information contact;
John Wanyancha
SBL Corporate Relations Director
Tel: 0692148857
Email: john.wanyancha@diageo.com
For Further information regarding project implementation contact;
Neema Kimaro
Communications and Campaign Specialist
WaterAid Tanzania
0713906221
Email: NeemaKimaro@wateraid.org
No comments:
Post a Comment