Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 15 March 2022

BODI YA WAKURUGENZI TRA YAVUTIWA NA UWEKEZAJI WA SBL

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), John Wanyancha (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) muda mfupi kabla ya ziara ya kutembelea kiwanda cha SBL Dar es Salaam kuangalia namna mfumo wa stempu za kielektroniki unavyofanya kazi katika kiwanda hicho.
Wajumbe wa wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mussa Ulledi wakielekea kwenye sehemu ya kufungashia (packaging area) kwa ajli ya kukagua utekelezaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki katika kiwanda cha Kampuni ya Bia ya Serengeti kilichopo Dar es Salaam.
Meneja Ufungashaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Praygod Minja akimwelekeza Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata namna mfumo wa stempu za kielektroniki unavyofanya kazi alipotembelea kiwa cha cha kampuni cha Dar es Salaam pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya TRA. Nyuma yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya SBL, Mark Ocitti.

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) cha Dar es Salaam na kuelezea kuridhishwa na uwekezaji inayofanya kwenye kampuni hiyo hapa nchini.

Akiongea katika ziara hiyo iliyolenga kuangalia namna zoezi la utekelezaji wa stempu za kielektroniki unavyoendelea, mwenyekiti wa bodi hiyo, Ulledi Mussa alisema uwekezaji unafanywa na SBL unatija kubwa kwa taifa.

“Upanuzi mkubwa wa viwanda vyenu unaonyesha kuwa mpo na mtanendelea kuwepo. Serikali ipo Nyuma yenu na changamoto mbali mbali za kikodi zitakuwa zikendelea kufanyiwa kazi ili kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kufanya bishara zenu,” alisema

Mwenyekiti huyo alisema kuwa TRA inaichukulia kampuni ya SBL km mdau muhimu wa maendeleo na kushukuru kwa uwekezaji wake katika miradi mbali mbali ya kijamii. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwekeza katika midari mbali mbali ya kijamii kama vile maji, elimu, Kilimo endelevu na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment