Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose. |
- Makubaliano yataongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za kidijitali katika mikoa ambayo haijafikiwa nchini
- Huduma hii itapatikana kupitia satelaiti yenye kasi kubwa ya EUTELSAT KONNECT
- Makubaliano haya yanafuatia mafanikio ya majaribio yaliyofanywa na Vodacom na Eutelsat kuonesha ufanisi wa teknolojia ya satelaiti
Huduma hii mpya itatoa fursa kwa wafanyabiashara binafsi na wa kimataifa, sekta ya utalii na hoteli ambapo mafanikio yameonekana katika majaribio yaliyofanikiwa kwa Vodacom Tanzania PLC kupanua wigo wa upatikanaji huduma na kuwafikia watumiaji ambao walikuwa hawajafikiwa awali. Huduma hizi zitatolewa na Vodacom huku vifaa vikiunganishwa na Konnect Africa.
Akizungumza wakati wa kutangaza mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Sitholizwe Mdlalose alisema, “Tunafuraha kubwa kujumuisha huduma zetu kwenye satelaiti hii, tukitumia uwezo wa satelaiti mpya kabisa ya EUTELSAT KONNECT ambayo itatuwezesha kutimiza dhamira yetu ya kufikisha huduma za mtandao katika maeneo yote nchini.”
Aliongeza kusema kuwa kwa kutumia KONNECT, Vodacom itapanua mtandao wake kufikia asilimia 100 ya eneo lote la Tanzania, yaani kuunganisha mikoa na wilaya zote na vijiji bila kujali umbali husika, “kwa huduma hii, tutaunganisha kila mtu, hii ni pamoja na maeneo ambayo hayajafikiwa hivi sasa, ikiwa na kasi ya hadi 100Mbps” alisema mkurugenzi huyo.
Huduma hii inaendana na dhamira ya Vodacom Tanzania kuboresha upatikanaji wa huduma za kidijitali zenye kasi kwa watu wengi zaidi nchini kwa kubuni njia mpya za kufikisha huduma kwa watumiaji wote.
Toka ianze kutoa huduma mwishoni mwa mwaka 2020 EUTELSAT KONNECT ni satelaiti mpya yenye kasi kubwa inayotoa huduma kwa kasi na viwango vinavyohitajika. Ina rasilimali kubwa inayowezesha utoaji huduma za kasi ikiwa na mtandao unaofikia karibu eneo lote la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, hii inawezesha moja kwa moja kwa watumiaji na wafanyabiashara kupata huduma ya intaneti yenye kasi zaidi.
Mojawapo ya mikakati ya Vodacom Tanzania Plc ni ushirikishwaji kwa wote katika kuondoa mgawanyiko kwenye upatikanaji wa huduma za kidijitali, hivyo ushirikiano huu una uzito mkubwa kwa Vodacom, kwani utatoa huduma kwa watu ambao hawajawahi kupata huduma za mtandao tangu tupate uhuru.
Akichangia kwenye makubaliano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Konnect Africa, Philippe Baudrier alisema, “Tuna furaha kubwa kushirikiana na Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza barani Afrika katika sekta ya mawasiliano, kwa kupanua wigo wa mtandao wake nchini Tanzania. Mkataba huu unaonyesha jinsi ambavyo uwezo mkubwa wa satelaiti ya EUTELSAT KONNECT unaweza kutimiza mahitaji makubwa kwa maeneo ya bara la Afrika ambayo hayajafikiwa au yenye huduma hafifu na ina ashiria mafanikio katika maendeleo ya usambazaji wa huduma baada ya makubaliano yetu nchini Nigeria, Afrika Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)”
Kuhusu Vodacom Tanzania PLC
Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya huduma za mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi wa data nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa watumiaji zaidi ya milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni zake ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inamilikiwa na Vodafone Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA
Kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.vodacom.co.tz
Kuhusu Eutelsat Communications
Eutelsat Communications, iliyoanzishwa mwaka 1977, ni moja kati ya makampuni yanayoongoza duniani ya satelaiti. Kupitia satelaiti zake dunia nzima pamoja na miundo mbinu ya ardhini, Eutelsat inawezesha wateja katika masoko ya Video, Data, Serikali na Mtandao wa Intanaeti kuwasiliana kwa tija na wateja wao bila kujali mahali walipo. Kuna takriban stesheni 7,000 za televisheni za makampuni kadhaa yanayoongoza yanayopitia Eutelsat kufikia watu Zaidi ya bilioni moja wenye vifaa vya DTH au walioungnaishwa mitandao ya ardhini. Ikiwa na makao makuu mjini Paris na yenye ofisi dunia nzima, Eutelsat ina wafanyakazi 1,500 kutoka nchi 50 ambao wanatoa huduma ya kiwango cha juu kabisa.
Kwa maelezo Zaidi juu ya Eutelsat, tafadhali tembelea: www.eutelsat.com
No comments:
Post a Comment