Benki ya NCBA Tanzania imechezesha droo ya kwanza ya sehemu ya kampeni yake inayojulikana kama ‘SHINDO LA AKIBA’ katika ofisi zake jinni Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Benki wa Rejareja na Bima ya NCBA Tanzania, Bw. Rahim Kanji amesema kuwa, “leo tunafanya droo yetu ya kwanza ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya ‘SHINDO LA AKIBA’. Kampeni hii tuliizindua mwezi Oktoba na tunatarajia itafika kikomo mnamo mwezi Desemba 2021. Kampeni hii itajumuisha wateja wetu wote lakini pia tunawakaribisha wale ambao hawajafungua akaunti kwetu wafanye hivyo ili kunufaika na kampeni hii pamoja na huduma zetu za kiakiba pamoja na nyinginezo nyingi.”
“Lengo kuu ni kuwahamasisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kujijengea utamaduni wa kuweka akiba badala ya kuhifadhi pesa taslimu majumbani. Mbali na usalama ambao unatolewa kwa kuweka akiba benki, pia tuna huduma za Akaunti ya Biashara ya Dhahabu ambayo ni maalum kwa biashara za kiwango cha kati wenye miamala inayokua na wangependelea kusimamia gharama za miamala katika akaunti zao. Hii ni mahususi kwa wateja ambao wanakuza biashara kwenda kiwango kikubwa na wana uhitaji wa benki ambayo watakua nayo. Dhamira yetu ni kuwasaidia wateja kukuza biashara zao huku tukisimamia mahitaji yao ya kibenki. Lakini pia ni sehemu ya kuwashukuru kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu kwa kipindi chote walichokuwa nasi, hususani tukiwa tunaelekea kuanza kwa msimu wa sikukuu mwezi ujao,” aliongezea Bw. Kanji.
“Zawadi ambazo tumezikabidhi leo ni sehemu ya zitakazokuwa zikitolewa kila mwezi ambazo ni pamoja na kulipiwa Dstv kifurushi cha premium kwa muda wa miezi mitatu kwa washindi wawili kila moja. Kupatiwa kadi ya malipo ya kujaza mafuta kwenye vituo tofauti kwa miezi mitatu kwa washindi wawili. Pia kila mwisho wa mwezi tutakuwa tunatoa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni moja kwa wateja wawili pamoja na vocha ya kufanya manunuzi kwenye ‘supermarket’ yenye thamani ya shilingi 450,000/- kwa wateja wawili. Na cha kusisimua zaidi katika kuelekea mwisho wa kampeni, kutakuwepo na zawadi kubwa ambapo mteja mwenye bahati atakabidhiwa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 10 za Kitanzania,” akihitimisha Mkuu wa Huduma ya Kibenki ya Rejareja na Bima wa benki ya NCBA Tanzania.
Kampeni ya ‘SHINDO LA AKIBA’ na benki ya NCBA Tanzania inajumuisha wateja wa benki hiyo wote na ambao sio wateja watakaokuwa tayari kufungua akaunti na kuhifadhi pesa. Benki ya NCBA ina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, na Visiwani Zanzibar. Ambapo kwa kipindi chote cha kampeni takribani wateja 18 watakuwa wakizawadiwa kila mwezi na kufanya idadi ya washindi wote kufikia 55 mpaka pale kampeni itakapofikia kikomo.
Ili kuweza kushiriki na kuibuka washindi wa zawadi mbalimbali wakati wa kampeni, wateja wa akaunti binafsi wanatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi milioni 10 za Kitanzania ndani ya mwezi na akaunti zao kutopungukiwa na kiasi cha shilingi 5 za Kitanzania ndani ya kipindi chote cha miezi mitatu ya kampeni. Pia kujiwekea nafasi kubwa ya kujishindia zawadi mbalimbali, wateja wanatakiwa kuwa na salio au kuweka kiasi cha pesa kinachohitajika kukidhi vigezo ndani ya kipindi cha kampeni.
Na kwa wateja wenye akaunti za wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kukidhi vigezo vya kushinda zawadi mbalimbali wakati wa kampeni, wanatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi milioni 100 za Kitanzania na akaunti zao kutopungukiwa na kiasi cha shilingi 50 za Kitanzania ndani ya kipindi chote cha miezi mitatu ya kampeni. Vilevile, ili kujiwekea nafasi kubwa ya kujishindia zawadi mbalimbali, wateja wanatakiwa kuwa na salio au kuweka kiasi cha pesa kinachohitajika kukidhi vigezo ndani ya kipindi cha kampeni.
Kwa wateja wa huduma binafsi za benki, Alireza na Aeman, pamoja na Sabri Omar Ali walizawadiwa kuunganishwa na kifurushi cha Dstv Premium kwa miezi mitatu kila mmoja. Yohana Joseph Maarifa na David Joseph Malikusema wao walipatiwa kadi ya mafuta yenye thamani ya kiasi cha shilingi 150,000/- za Kitanzania ambayo wanaweza kuzitumia kwa kipindi cha miezi mitatu kila mmoja. Wakati huo huo William Nicholous Mpanji aliondoka na vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi 450,000/- za Kitanzania huku Benard Manyeruke alizawadiwa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni moja.
Wafanyabiashara wadogo na wa kati nao hawakuachwa nyuma, Huafa Textiles Co Ltd na Yukon General Trading Company Limit walizawadiwa kuunganishwa na kifurushi cha Dstv Premium kwa miezi mitatu kila mmoja. Kika Construction Company Limited na Dongsheng Motors International Co wao walipatiwa kadi ya mafuta yenye thamani ya kiasi cha shilingi 150,000/- za Kitanzania ambayo wanaweza kuzitumia kwa kipindi cha miezi mitatu kila mmoja. Wakati huo huo Arusha Art Limited waliondoka na vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi 450,000/- za Kitanzania huku OGEFREM walizawadiwa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni moja.
NCBA inajivunia kuwa benki ya Kiafrika ikifanya shughuli zake katika viwango vya kimataifa, NCBA Group ni miongoni mwa mtandao mkubwa ya benki zenye idadi kubwa ya wateja Afrika ikiwa na msingi imara wa wateja zaidi ya bilioni 40 barani kote na kwenye ukanda huu, ikiwa imejizatiti katika huduma za kimtandao, pamoja na ukwasi wa uliojitosheleza kwenye kutoa huduma za kifedha. Benki ya NCBA Tanzania Limited kwa sasa ina matawi 12 nchini Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment