Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Thursday, 11 November 2021

DCB YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Uhuru, Dorice Mawole (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na DCB katika banda la benki hiyo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
Meneja Mahusiano Wateja Binafsi wa Benki ya DCB, Manibakhila Kambinda (kulia), akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja kuhusu huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na akaunti ya elimu ya DCB Skonga inayomwezesha mteja kuwa na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufika Chuo Kikuu. Ilikuwa ni katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Uhuru, Dorice Mawole (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na DCB ikiwa ni pamoja na kampeni inayoendelea ya Sinia la DCB yenye lengo la kuwafanya wateja kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba huku wakifurahia zawadi nono kutoka kwenye sinia ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, zawadi za vocha, simu za mkononi kwa watakaokidhi vigezo. Ilikuwa ni katika banda la benki hiyo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Uhuru, Dorice Mawole (katikati), akipozi mbele ya wapigapicha pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika banda lao wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment