Wadau pamoja na wataalam wa huduma za fedha nchini wamesema Tanzania ipo miongoni mwa nchi zilizopo kwenye jangwa la sahara ambazo zina idadi ndogo sana ya wananchni wanao tumia huduma za kifedha licha ya ujio wa huduma za simu benki na wakala wa benki kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hizo asilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini baado kuna kazi kubwa ya kutoa elimu ili kukuza ulewa kwa watanzania kuhakikisha wanafaidika na utumiaji wa huduma za kifedha ambapo Benki ya Biashara ya Tanzania TCB imejipanga kimkakati kwa ajili yakutoa elimu ya kifedha nchi nzima ili kuleta tija na hamasa kila mtanzania aweze kutumia huduma hizo.
Akitoa taarifa hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara ambazo utafiti uanonyesha ina kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi wake kuelewa umuhimu wa kutumia huduma za fedha licha ya ujio wa Taasisi nyingi za kifedha pamoja na mawakala wa benki mbalimbali kuongeza idadi ya watumiaji wa uhuduma za kifedha. Ameongeza kwa kusema kwa asimilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita bado idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine ambazo hazipo kwenye ukanda huo kwa hiyo ni muhimu kwa wadau wa fedha kuendelea kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya watumiaji.
Aidha Moshingi ameongezea kuwa utafiti uanonyesha suala la uelewa mdogo wa masuala ya uhuduma za kifedha ndio sababu inayopelekea wananchini wengi wanaoishi kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania kuogopa kutumia huduma za kifedha kwa kuamini sio huduma zinazoweza kumkomboa mtu wa kipato cha chini lakini kupitia juhudi zilizoanza kuchukuliwa na serikali anaamini wananchi wengi watapata muamko wa kutuia huduma hizo ikiwemo huduma za bima.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yameanza toka Novemba 8 hadi Novemba 14 mwaka huu, yanalenga wadau mbalimbali wakiwemo; watumishi wa umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs), asasi za kiraia, wahariri na waandishi wa vyombo vya habari, watoa huduma za fedha na umma kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia Fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.
Amesema Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji Biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB, Deo Kwiyukwa amesema benki hiyo imeshiriki katika maonesho hayo ili kuweza kutangaza huduma wanazozitoa ili kuweza kupanua wigo kwa wananchi hasa wajasiriamali wadogowadogo.
Pia amesema TCB wanatoa huduma za kifedha kama vile kufungua akaunti, huduma ya benki kwa njia ya wakala, kubadili fedha za kigeni, bima, mikopo pamoja na kuinua biashara zinazowahusu wanawake hii yote ikiwa ni kuwafikia wananchi wote na kutoa huduma iliyo bora.
No comments:
Post a Comment