- Maadhimisho ya Wiki ya Usalama hufanyika kila mwaka katika nchi zote za Vivo Energy.
Kila mwaka kampuni ya Vivo Energy inaadhimisha wiki ya usalama, ikiwa na lengo la kuhamasisha wafanyakazi na washirika mbambali juu ya umuhimu wa usalama wa mazingira, barabara na afya yaani HSSEQ (Health, Safety, Security, Environment & Quality).
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni, “UWEZO + UTAYARI = USALAMA”. Kampuni ilitoa nafasi kwa wadau kutoa shuhuda za jinsi kanuni na taratibu za usalama zilizopo zinachangia mafanikio katika biashara. Zaidi ya shududa 1200 zilitolewa zikigusa mazingira, afya, bidhaa bora, ushindani, usalama na ulinzi.
Mifano na shuhuda zilizoongoza kwa uboreshaji wa usalama kwenye makundi yote kwa ujumla yalichukuliwa na kusambazwa kwenye kampuni nzima kuhamasisha wengine kuiga mfano wa zoezi hilo.
Akitoa maoni siku hiyo, Grant Bairstow, Kiongozi wa HSSEQ Vivo Energy alisema “Usalama ndo kitovu cha biashara na mafanikio yetu kwa muda mrefu hapa Africa. Nina Furaha kutoa ripoti ya kwamba tunaendelea kufanya vizuri kwa kuzingatia yote yaliyo muhimu kwetu kupitia HSSEQ kwa mwaka huu.”
Bi. Khady Sene, Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania aliongeza, “Lengo letu ni kuendeleza utamaduni wa kujali usalama katika maeneo yote ya biashara. Mwaka huu, Vivo Energy Tanzania imeshirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabani katika kutoa elimu kwa madereva pikipiki pamoja na utoaji wa viakisi mwanga (reflector jacket) katika vituo 10 Dar es Salaam, yaani Mwembe-yanga, Vijibweni, Kipunguni, Pugu, Goba, Mikocheni, Masaki, Ubungo, Mbezi Beach na Bunju’’
Vivo Energy inazidi kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo yake ya HSSEQ ili kupata matokeo chanya na endelevu sambamba na shabaha yake ya kuwa kampuni inayoheshimika zaidi Afrika katika sekta ya nishati.
Media contact:
Grace Kijo
+255754711460
Grace.Kijo@vivoenergy.com
Kuhusu Vivo Energy
Kampuni ya Vivo Energy ilianzishwa mwaka 2011 ikiwa na shabaha ya kuwa kampuni inayoheshimika zaidi Afrika katika sekta ya nishati. Katika kipindi cha miaka kumi tu, Vivo Energy imefanikiwa kueneza shughuli zake katika nchi 23 za Afrika. Kampuni imeajiri zaidi ya wafanyakazi 2,700 na ina nafasi ya mita za ujazo zaidi ya 1,000,000 ya kuhifadhia mafuta. Kampuni ni ya Ubia, kati ya Shell na Vivo Lubricants B.V, vyanzo, mchanganyiko, vifurushi na usambazaji wa bidhaa zenye chapa za Shell na Vilainishi kwenye viwanda ndani ya nchi sita.
Vivo Energy Tanzania, ilianzishwa mwaka 2019 ikiwa na leseni ya kumiliki chapa ya Engen katika uuzaji na usambazaji wa petroli na diseli. Na chapa ya Shell katika uuzaji na usambazaji wa vilainishi vya Shell.
Sambamba na bidhaa hizi, vituo vya Engen vinawapa wateja huduma za migahawa na maduka ya kisasa pamoja na maeneo ya kusafisha magari.
Mpaka sasa, Vivo Energy Tanzania ina miliki vituo 35 na inategemea kufikia vituo 45 ifikapo Disemba mwaka 2021.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Vivo Energy, naomba utembelee tovuti yetu www.vivoenergy.com
No comments:
Post a Comment