Baadhi ya mabalozi wa Kampeni ya 'Sinia la DCB', wakipozi mbele ya wapigapicha muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo, jijini Dar es Salaam. |
- WATEJA KUZAWADIWA ZAWADI NONO KILA MWEZI.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa DCB, Fortunata Benedict alisema uzinduzi wa Kampeni ya Sinia la DCB ni moja ya zawadi kabambe tuliyowaletea wateja wetu ikiwa ni moja ya hatua za kuonyesha shukurani zetu kwa wateja wetu wanaoendelea kutuunga mkono kwa kufanya biashara na DCB.
Alisema Kampeni ya Sinia la DCB itadumu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Mwezi Novemba ambapo wateja wa zamani na wapya watashiriki, lengo kubwa ni kuwafanya wateja wa DCB kudumisha utamaduni wa kujiwekea akiba huku wakifurahia zawadi nono kutoka kwenye sinia ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, vocha za zawadi, simu za mkononi kwa watakaokidhi vigezo.
“Kama mjuavyo kipindi hiki tunaanza shamrashamra za mwisho wa mwaka, sisi kama DCB tumeonelea kuwaletea kampeni hii ili kuonyesha shukurani zetu kwa wateja wetu kwa ushirikiano wanaotupa kwa kujiunga na huduma na bidhaa zetu mbalimbali zilizopo sokoni.
Bi Fortunata alizitaja bidhaa zitakazokuwemo ndani ya Sinia la DCB “Kama neno lenyewe liitwavyo ‘Sinia’ ITAKUWA Sinia kweli kweli, kwani ndani ya sinia kutakuwa na bidhaa mbalimbali za DCB kama akaunti ya Skonga, akaunti za mshahara, akaunti ya WAHI, DCB KIBUBU,ambazo wateja wetu wa zamani watahitajika kuweka amana kwenye akaunti zao na wapya watahitajika kufungua akaunti za kwenye sinia ili kuweza kufurahia zawadi zetu tutakazotoa kila mwezi”, alisema.
Akizungumza jinsi ya kushiriki katika kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zakaria Kapama alisema Kwa wateja wenye kupitisha mishahara yao DCB na kuweka amana kwa wingi kuliko wote ya kuanzia TZS 300,000 kwa muda wa mwezi mmoja atajishindia zawadi ya simu aina ya Samsung kila mwezi. Aliongeza kwa mteja wa kibubu (wa zamani na mpya) ambae wataongoza na kua na amana kubwa ya kuanzia milioni moja na za zaidi kwa muda wa mwezi mzima atajishindia voucher ya manunuzi kwa ajili ya krismasi na mwaka mpya ambapo washindi watajishindia zawadi mbalimbali za kuvutia ikiwemo simu za mkononi na pesa taslimu.
Aidha Bwana Kapama alisema wateja wapya wa akaunti ya Skonga wenye mpango wa mwezi wa kiasi cha sh 300,000 na zaidi akaunti zao zitaongezwa kiasi cha sh 300,000 kila mmoja kama bonasi. Aliongeza, kwa wateja wa akaunti ya WAHI ambao watafungua akaunti na kuweka amana kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea, kwa mteja atakae ongoza kuwa na amana nyingi atajishindia kiasi cha pesa hadi shilingi milioni moja.
Aidha Bwana Kapama alisema kutakuwa na washindi watatu kila mwezi kwa wateja wapya ama wa zamani wa akaunti huku mteja atakayeongeza amana kila wakati katika muda wote wa kampeni akijiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuzawadiwa. “Utakuwa ni msimu wa furaha na shangwe kwa wateja wetu huku washindi wenye amana za juu kila mwezi wakijishindia vocha za manunuzi kwa ajili ya sikukuu ya Christmas”, alisema Bwana Kapama.
Kama tulivyosema zawadi hizi ni ishara tu ya kuonyesha shukurani zetu kwa wateja wetu, tunatoa wito kwa wateja wetu wa zamani na wapya kushiriki katika kampeni hiii ili kufurahia zawadi hizi nono lakini kilicho bora zaidi ni kufaidika na manufaa yaliyo katika bidhaa hizi zinazopatikana ndani ya Sinia la DCB”, aliongeza Bwana Kapama.
No comments:
Post a Comment