BENKI YA CRDB YANOGESHA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI NCHINI (TAPIE)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA) kwa udhamini wa Benki ya CRDB, ambapo alisema kuwa Benki hiyo imeiweka sekta ya elimu katika moja ya vipaumbele vya uwezeshaji, ikiwa ni sehemu za kusaidia jitihada za Serikali pamoja na wadau wa sekta hiyo kuboresha mazingira ya elimu nchini, ili kuweza kutoa elimu bora itikayopelekea taifa kuzalisha rasilimali watu iliyo bora katika nyanja mbalimbali. Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Blue Sapphire, Mbezi Beach, Dar es salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipokea zawadi ya Keki kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA), Mahmoud Mringo ikiwa ni sehemu ya shukrani zao kwake kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Blue Sapphire, Mbezi Beach, Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Albert Katagira. Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA), Mahmoud Mringo akizungumza wakati akitoa salamu za Chama chao kwa mgeni rasmi, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA) uliodhamini na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye Ukumbi wa Blue Sapphire, Mbezi Beach, Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo cha Huduma za Uwakala wa Benki ya CRDB, Erick Willy akiwasilisha mada katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAPIA) uliodhamini na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye Ukumbi wa Blue Sapphire, Mbezi Beach, Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment