Baadhi ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia kwa umakini kwenye mkutano huo. |
Thierry Mouanza Dongala, ambaye ni mwanzilishi wa taasisi ya Accountable Africa, ambao ni waandaaji wa kongamano hilo, anasema kuwa jukwaa hilo limekuja wakati sahihi kutokana na mada mbalimbali zinazojadiliwa. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji, Mheshimiwa Kitila Mkumbo, akiwataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi.
Mkurugezi wa taasisi ya ushauri ya MiDA Advisors, Aymeric Saha, inayotoa ushauri kwa baadhi ya taasisi kubwa za wawekezaji nchini Marekani zinapokuja kuwekeza Africa katika miradi ya miundombinu anafafanua kuwa kuna bilioni mia moja ambazo zimetengwa na taasisi wawekezaji kwaajili ya miradi endelevu ya miundombinu . Baadhi ya wawekezaji wengine walioshiriki katika mkutano huo walisisitiza juu ya serikali kuunga mkono wawekezaji kwa kuboresha mazingira.
Sekta ya Kilimo ilijadiliwa kwa mapana zaidi kwa wawekezaji wa kigeni kuonesha nia ya kushirikiana na wadau wadogowadogo wa Kitanzania ili kuongeza tija kwa lengo la kuongeza uzalishaji usiotegemea mbegu za GMO.
Peter Schuurs, Mwanzilishi wa taasisi ya reap, anasema, “Tunatamani kuona tunaweka mtaji wetu na kufanya kazi kwa bidii kwenye ardhi ya Tanzania ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na hasa lile la kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula katika kila mkoa kwa mtindo wa uwajibikaji endelevu"
Kongamano hilo pia liliwahusisha wawekezaji wa diaspora ambao hivi karibuni walirejea Africa kwa lengo la kutaka kuwekeza na hasa nchini Tanzania. Wanasema kuwa ni jukumu lao kuweka mtaji waliopata katika nchi za nje kufanya kazi Afrika na kwamba italeta faida zaidi. Wanafanya mazungumzo na kituo cha uwekezaji ili kusaidia kuhamisha mitaji yao ambayo ni zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.9 kutoka Ghana ifikapo mwaka wa fedha wa kimaifa.
MAWASILIANO:
Info@accountableafrica.com
No comments:
Post a Comment