Meneja wa Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (katikati), akizungumza wakati wa hafla hiyo. |
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba commercial (ACB), Dora Saria Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Choose to Challenge" yaani Chagua Changamoto zaidi kwa maana kuwa changamoto mara nyingi zinaleta fikra mpya, mitazamo mipya na mabadiliko.
Saria amesema, wanatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii bora ndio maana zaidi ya asilimia 50 ya wateja wanaopata huduma kwenye benki yao ni wanawake.
"Asilimia 50 ya wateja wetu ni wanawake ambao wamewezeshwa kwa kupewa huduma mbalimbali ambazo zimewasaidia kubadilisha hali zao za maisha kwa kuwa na maisha bora," amesema Saria.
Akiba Commercial Bank kama sehemu ya jamii pia inalichukulia swala hili kwa umakini na uzito wake tunaelewa na tunatambua na kuheshimu nafasi ya Mwanamke katika jamii.
Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Fata Vicoba Endelevu ambae pia ni mteja wa benki hiyo Hanipha Tarimo amesema amekuwa mteja wa Benki ya ACB kwa kipindi cha muda wa miaka mitano na ameweza kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara yake ya kuuza nywele origino za kike, maduka ya Nguo yaliyopo karioo mtaa wa msimbazi, na ameendesha maisha yake vizuri tokea aanze kutumia Benki hiyo.
Amesema, anawasihi wanawake wengine wasisite kuchukua kuitumia Benki ya Akiba Commercial Bank kwani inasaidia kuinua wanawake kiuchumi na pia ACB wamekuwa ni moja ya taasisi wasikivu hususani pale mteja anapokua amekwama.
No comments:
Post a Comment