- Kulipa na Airtel Money ni njia ya uhakika na salama.
Akizungumza leo jijini Dar Es Salaam, Meneja wa Airtel Money, Philemon Matoi amesema, "kumlipia mtoto karo ya shule kupitia Airtel Money ni nafuu na salama , kwani ndani ya dakika chache unakuwa umefanya malipo bila ya kutoka nyumbani. Hili ni suluhisho kwa wazazi wote na mashule kwa ujumla. Sisi sote tunafahamu kuwa mwezi wa Januari ni moja ya miezi yenye shughuli nyingi kwa wazazi au walezi kwa kulipa karo za shule kwa watoto wao. Hivyo, Natoa wito kwa wateja wa Airtel Money na Watanzania wenzangu kwa ujumla, kutumia Airtel Money kama njia rahisi katika kufanya malipo, ya haraka, salama na ya kuaminika, aliongeza Matoi.
Ili mtu alipe ada ya shule kwa kutumia Airtel Money, anapaswa kufuata hatua zifuatazo
- Piga *150*60 # kupata orodha yako ya Airtel Money
- Chagua 5 - Fanya Malipo
- Chagua 4 - Weka Namba ya Kampuni (Namba ya Malipo ya Shule)
Akiongea katika hafla hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kings Anthony Bizulu alisema, “Lipa Ada na Airtel Money ni huduma rahisi na ya haraka kwetu, kwani inatupa urahisi kwenye kukusanya karo ya shule na michango mingine, bila ya kuwa na kazi ya ziada ya makaratasi au kupanga risiti kama ushahidi wa malipo. Pamoja na Airtel Money Lipa Ada, shule hutazama miamala kupitia mfumo ambao hufanya utunzaji wa rekodi kuwa rahisi sana, kupata ufafanuzi wa wanafunzi ambao wamelipa na ambao hawajalipa. Hapa Kings, tunatumia malipo ya ya Airtel Money kwa majukumu mengine muhimu, kama vile kutunza mahesabu, malipo ya mishahara ya walimu, malipo ya wauzaji, ambapo inaleta unafuu katika uongozi wa shule”.
- Ingiza Kiasi
- Ingiza namba ya kumbukumbu (Jina la Mwanafunzi & Daraja / Namba ya Kitambulisho cha Mwanafunzi)
- Ingiza namba ya siri.
Anthony aliongeza akisema,”Ningependa kuhamasisha shule zingine zitumie huduma za Lipa Ada na Airtel Money katika shughuli zao za malipo kwani ni huduma inayofaa zaidi, ya uwazi na ya kuaminika kwa masuala ya kifedha. Huduma hii inasaidia kufanya maamuzi, kupanga na kutabiri kwa kutumia simu yako ya kiganjani.
Nae mmoja wa mzazi katika Shule ya Kings, John Kadege alisema, “siku zote nimekuwa nikitumia huduma ya Airtel Money Lipa Ada katika kulipa karo ya watoto wangu hapa shuleni, kwani inanipa unafuu wa kulipa karo ya shule wakati wowote na mahali popote. Pia ni njia yenye usalama, inasaidia kuokoa muda na rasilimali ikilinganishwa na njia zingine za kawaida ambazo zinapoteza muda kwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine .”
Airtel Money Tanzania kwa sasa imeunganishwa na zaidi ya wauzaji 1000 wakiwemo watoa huduma za maji, umeme na mengineyo, na pia imeunganishwa na zaidi ya taasisi 40 za kifedha ambazo huruhusu wateja kutoa pesa na kuweka akiba. Kwa kuongeza, Airtel Tanzania inapanuka kwa kasi zaidi hata nchini na mpaka sasa zaidi ya maduka 800 ya Airtel Money yanayotoa huduma na bidhaa zote za Airtel hapa nchini.
No comments:
Post a Comment