Akizungumza wakati wa utoaji elimu huo, ulioambatana na ufunguaji wa akaunti mbalimbali zilizo chini ya mwamvuli wa WAJIBU, Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza - Hildegard Mung'ong'o, alisema elimu waliyopewa watoto hao ililenga kuwajengea utamaduni endelevu wa kuweka akiba tangu wakiwa wadogo.
Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza, Hildegard Mung'ong'o akiangalia jinsi mtoto Myreen Rashid akiweka pesa ikiwa ni sehemu ya kujifunza kuhusu kuweka tangu wakiwa watoto. |
Watoto wakiwa katika Tawi la Benki ya NMB Oyster Plaza wakipata elimu ya fedha. |
Mameneja hao waliwataka wazazi na walezi kujitokeza matawini kufungua akaunti za watoto ambazo licha ya kadi ya Benki kuwa nayo mtoto, mzazi atabaki kuwa msimamizi mkuu wa akaunti kwa kutambua miamala inayofanyika.
NMB kupitia WAJIBU, imelenga kuwa na taifa la kesho lenye uelewa wa kina wa elimu ya masuala ya fedha, ndio maana ikaanzisha mpango maalumu unaowajumuisha mzazi na mtoto, wakiamini wateja hujengwa tangu wakiwa wadogo.
No comments:
Post a Comment