Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 30 November 2020
KIVUMBI CHA #EPL BADO KINAENDELEA LEO USIKU NDANI YA DStv
Kivumbi cha #EPL⚽⚽ bado kinaendelea usiku leo ndani ya DStv, hakikisha unalipia kifurushi chako cha Compact TShs 49,000 kwa kupiga *150*53# tu uweze kutazama mechi hizi au 0659 07 07 07 kujiunga kwa gharama nafuu TShs 79,000 tu upate kifurushi cha Family mwezi mmoja bure.
#VibeLaSikukuunaDStv
#SokaLisilopimika
TIGO YAENDELEA KUKABIDHI ZAWADI ZA SIMU KWA WASHINDI MBALIMBALI WA #JazaTukujazeTena
TunakabidhiTena: Tigo yaendelea kukabidhi zawadi za Simu kwa washindi mbalimbali wa #JazaTukujazeTena ambapo wateja hujishindia pia bonus za dakika, MB na SMS na kubwa zaidi kupata Simu Janja. "Bado tunaendelea kutoa simu kwa wateja wetu ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote. Wanachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi wapate bonus na zaidi wanaingia kwenye droo ambapo wanaweza kushinda simu janja mbalimbali" Joseph Mutalemwa-Mkurugenzi wa Tigo kanda ya pwani. @jotiofficial |
"Mbali na Bonus wanazojipatia wateja wetu kila siku pindi wakijiunga kifurushi pia wanajiwekea nafasi ya kushinda simu janja ikiwemo Samsung Note 20 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2" Joseph Mutalemwa - Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani. |
Amani Adami kutoka Kiwalani Dar es salaam ndiye mshindi wa Samsung Note 20. Mshindi mmoja kati ya watatu wa wiku hii. Ukiwa na Tigo wewe ni mshindi. Nunua kifurushi chochote na Tigo itakupa Bonus za Dakika, SMS na Mb's na kubwa zaidi utajiwekea nafasi ya kushinda smartphone kila siku. #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 Tatu kila wiki. Joseph Mutalemwa - Mkurigenzi wa Tigo kanda ya Pwani pamoja na @jotiofficial wakimkabidhi simu. |
"Huu mzigo ukiibiwa huu lazima uweke msiba huu maana ni balaa, bei yake ni balaa" @jotiofficial Ukinunua kifurushi Tigo unapata Bonus za Dakika, SMS na MB's na zaidi unajiwekea nafasi ya kushinda smartphone #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 tatu kila wiki. #JazaTukujazeTena |
Mama Kashinda! Hongera wewe ni mmoja wa washindi wa Itel T20 wiki hii @jotiofficial Bado wengine Wengi. Nunua kifurushi chochote na Tigo itakupa Bonus za Dakika, SMS na Mb's na kubwa zaidi utajiwekea nafasi ya kushinda smartphone kila siku. #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 Tatu kila wiki. |
BURE: Ukinunua kifurushi kutoka Tigo unapata Bonus ya MB, SMS au Dakika na zaidi unapata Burudani kali kutoka kwa wasanii kibao kwenye tamasha la Wasafi Tumewasha na Tigo kesho uwanja wa Taifa-Kahama. Piga *147*00# kujiunga. @wasafitv #TumewashaNaTigo #JazaTukujazeTena |
AIRLINK YAZINDUA SAFARI MPYA DAR - JOHANNESBURG
Airlink ikiwa imepaki uwanja wa ndege wa O.R Thambo Afrika Kusini. |
Muonekano wa ndani wa ndege ya Airlink. |
Huduma ya chakula. |
Huduma ya vinywaji. |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Rodger Foster alisema wameanzisha huduma mpya kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kukuza fursa za kiuchumi.
"Airlink ina furaha kuanzisha huduma za moja kwa moja za ndege zetu ili kukuza biashara na utalii kwa kuwa sehemu hizi mbili zinafanana kwa namna moja ama nyingine katika mambo hayo," alisema.
PRESIDENT MWINYI CALLS FOR GOVERNMENT, FINANCIAL INSTITUTIONS PARTNERSHIP
President of Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi, has called on financial institutions and local development partners to work with the government to bring about significant change for the benefit of the people.
President Mwinyi was speaking during a special seminar organised by CRDB Bank to highlight various opportunities offered by the bank and discuss how best to work together between the government and the lender in achieving development projects in the country and move banking services closer to citizens to stimulate economic growth.
STANDARD CHARTERED BANK, SANLAM LAUNCH BANCASSURANCE PRODUCTS
The joint business venture aims at serving customers who want to widen the scope of insurance service penetration that ensures the security and safety of their properties and motor vehicles.
BENKI YA NMB TAASISI KINARA KUSAIDIA JAMII ELIMU NA AFYA
Benki ya NMB imetajwa kuwa taasisi kinara ya kifedha katika Manispaa ya Ilala mkoani Dar es salaam inayotumia kiasi kikubwa cha pato lake kuisaidia jamii katika Nyanja za Elimu na Afya kupitia Mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Kupitia mpango huo Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kati ya taasisi nyingi za fedha kwenye mkoa huo, ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali kuhakikisha huduma bora za kiafya na elimu zinapatika kwa wananchi.
Hatua hiyo ilipelekea Manispaa hiyo kuipatia Benki hiyo cheti cha Pongezi, kwenye hafla ya kufunga kongamano la siku ya mlipakodi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika hafla hiyo, Manispaa ya Ilala ilikabidhi vyeti kwa taasisi, mashirika, makampuni na wafanyabiashara 100 Bora wa Ulipaji Kodi Bila Shuruti, huku NMB ikipongezwa na kutunukiwa kama Kinara wa matumizi ya pato lake katika kusaidia jamii.
Sunday, 29 November 2020
UBALOZI WA TANZANIA AFRIKA KUSINI WAPEWA CHANGAMOTO YA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI, SIASA
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano. |
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akiendesha kikao na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini. |
Na Nelson Kessy, Pretoria
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini wapewa changamoto ya kuhakikisha kuwa unatekeleza Diplomasia ya Uchumi pamoja na Diplomasia ya Siasa iliyopo ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM (2020-2025).
Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge wakati alipotembelea Ubalozi huo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujionea utendaji kazi wa Ubalozi na mali za Serikali nchini humo.
Balozi Ibuge ameutaka Ubalozi huo kuhakikisha kuwa unatekeleza diplomasia ya uchumi pamoja na diplomasia ya siasa kwa weledi ili kuleta manufaa ya Taifa.
"Nawapongeza kwa utendaji kazi wenu na nawasihi muendelee kujituma katika kazi (proactive) katika kuwapata wawekezaji na kutengeneza kuwa ni sehemu ya mfumo wa kuleta mabadiliko ambayo Serikali imeyapanga kupitia Ilani ya CCM ya 2020-2025," Amesema Balozi Ibuge.
Saturday, 28 November 2020
SADC-TROIKA, UN KUBORESHA MFUMO WA USALAMA NDANI YA DRC
Akithibitisha kuhusu mashirikiano ya mfumo wa kuimarisha ulinzi na usalama nchini DRC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika mkutano huo amesema kuwa kamati ya utatu inayoshughulika na usalama ndani ya jumuiya ya SADC imekutana kwa dharura ili kuweza kuangalia namna ya kukabiliana na matishio ya ugaidi yanayotishia sana hali ya amani na usalama katika nchi zilizopo ukanda wa SADC ikiwemo Msumbiji, Congo DRC na Tanzania.
Friday, 27 November 2020
ASSOCIATION OF TANZANIA EMPLOYERS ORGANISES A MEETING OF FEMALE FUTURE ALUMNI NETWORK MEMBERS
7 TRILLION TO LIFT ZANZIBAR BLUE ECONOMY
Zanzibar - Zanzibar based Salmin Fisheries Limited has secured 3bn US Dollar (about 7 trillion Shillings) business partnership in the construction of fish processing industries and a fish landing port.
Salmin Fisheries Executive Director, Dr. Salmin Ibrahim said here yesterday that Turkish Northland Capital Investments is willing to invest the amount in the ambitious projects under the Government spearheaded Blue Economy.
The indigenous fishing firm and Equity Bank have teamed up under a strategic programme to support small-scale fisheries through training, financing and marketing.
KCB GROUP SIGNS DEAL TO BUY TWO BANKS IN RWANDA, TANZANIA
KCB Group CEO Joshua Oigara. |
KCB Group has signed a deal with London-listed financial services firm Atlas Mara Limited to buy stakes in it's banking units in Rwanda and Tanzania, its chief executive Joshua Oigara announced on Thursday.
The proposed transaction will see Kenya’s biggest lender by assets acquire Banque Populaire du Rwanda Plc (BPR) and the African Banking Corporation Tanzania (BancABC), strengthening its business in the two countries.
Under the proposed deal KCB will the acquire a 62.06 per cent stake in Banque Populaire du Rwanda Plc and a 100 per cent stake in African Banking Corporation Tanzania.
The transaction is subject to obtaining shareholder and regulatory approvals in Rwanda and Tanzania.
In a statement, Mr Oigara said the transaction is part of KCB’s "ongoing strategy to explore opportunities for new growth while investing in and maximising returns from the Group’s existing businesses."
The acquisition, he added, will buttress the Group’s leadership position and give it a stronger edge to play a bigger role in driving the financial inclusion agenda in the East African region while building a robust and financially sustainable organization.
KAA MKAO WA PIRA BIRIANI WIKIENDI HII KUTAZAMA MICHUANO YA EPL NDANI YA DStv
Kupitia Vibe La Sikukuu na DStv kama DStv, piga 0659 07 07 07 kujiunga kwa TShs 79,000 tu na upate ofa ya kifurushi cha Family.
MAKATIBU WAKUU SADC - TROIKA WAKUTANA KUJADILI SIASA NA USALAMA
Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone, Botswana.
Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).
Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.
Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae mjini Gaborone.
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA ukiendelea. |
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia mkutano. |
MAWAZIRI SADC - TROIKA WAKUTANA KWA DHARURA BOTSWANA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Dkt. Lemogang Kwape akifungua mkutano wa Dharura wa baraza la mawaziri, kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax. |