Wafanyakazi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja vivi karibuni katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. |
Timu ya mpira wa miguu ya MultiChoice Tanzania na KCB Bank katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mtanange wa kukata na shoka baina yao. |
Mpambano kati ya timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) na KCB Bank katika mchezo wao maalum wa ‘Wiki ya Huduma kwa wateja’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam hivi karibuni. |
Wameungana kuendeleza shamra shamra za wiki ya huduma kwa wateja kwa kufanya matembezi maalum pamoja na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu pamoja na michezo mbalimbali mapema leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika viwanja vya Gymkhana Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja MultiChoice Tanzania, Bi. Ngwitika Mwakahesya alisema kuwa “Wiki hii huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, lakini kwetu MultiChoice kila siku tunazingatia swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wetu wote kwa viwango vinavyotakiwa.“Mwaka huu MultiChoice tumeipa wiki hii kauli mbiu “Exceeding Customers Expectations” tukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wote imani katika huduma kwa kuwapatia huduma zenye ubora wa hali juu.
Katika mwezi huu pia MultiChoice tunatambua umuhimu wa wadau mbalimbali ambao tunashirikiana nao katika shughuli za kila siku za kibiashara hivyo tumezingatia hilo na ndiyo maana leo tuko hapa na wenzetu wa Benki ya KCB kwa ajili ya kushiriki michezo mbalimbali hususani mbio za kilometa 5 na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu iliyodhamiria kuboresha mahusiano baina yetu.
Mbali na shamra shamra hizi pia, napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wateja wetu juu ya huduma zetu mbadala ambazo zimelenga kuleta ufanisi na kuwapatia urahisi endapo watakua wanahitaji huduma kwa haraka ikiwemo kuangalia salio, kulipia kifurushi na kubadlisha aina ya kifurushi anachotumia. Wateja wetu wanaweza kupata huduma hizo kwa njia ya WhatsApp kupitia namba 0677 666 111, kwa njia ya USSD kwa kubonyeza *150*53#, kwa wateja wetu wenye simu za kidigitali wanaweza kuapata huduma zetu pia kwa kupakua App ya MyDStv. Hivyo mteja wetu anaweza kupata huduma akiwa nyumbani kwake kwa haraka Zaidi.
Alimaliza kwa kueleza kuwa mteja wa DStv pia anaweza kuendelea kufurahia huduma mbalimbali zinazopatikana katika kifurushi alichokifanyia malipo kupitia huduma ya DStv Now mahali popote kupitia simu yake ya mkononi, Laptop pamoja na Tablet mbali na huduma anayoifurahia kupitia televisheni yake awapo nyumbani.
No comments:
Post a Comment